📌JASMINE SHAMWEPU
Aidha jeshi hilo
limevitaka vyombo vya habari na mitandao ya kijamii vilivyoripoti habari hiyo kwa kuweka picha za vijana wa JKT ambao siyo wahusika wa habari hiyo,kuomba
rambi na kuondoka picha hiyo mara moja.
"Kabla ya kuanzia mafunzo vijana hufanyiwa usaili wa nyaraka zao pamoja na vipimo vya afya ili kufahamu utimamu wa mwili"amesema Mabena
Mabena amesema vijana ambao majibu ya vipimo vyao huwa na changamoto za kiafya hufanya mafunzo yao chini ya uangalizi wa wakufunzi ili kuhakikisha wanamalizia mafunzo yao salama.
"Kwa kuwa Hilo ni
kundi la lazima,vijana wenye ulemavu wa kuonekana Kwa macho hupokelewa Katika
kikosi Cha Ruvu JKT ambacho kina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.
Kadhalika amesema JKT
inasisisitiza kuwa kigezo Cha afya Cha vijana hao wa kundi la lazima wanakuja
makambini wakiwa na changamoto za kiafya kinazingatiwa Kwa kuwaweka chini ya
ulinzi.
Aidha amesema JKT
inazingatia sheria kanuni na taratibu za kitabibu sambamba na kuzingatia Mila
na desturi za Nchi yetu Katika kutekeleza jukumu lake la msingi la malezi ya
vijana.
"JKT linapenda
kutarifu uma kuwa mafunzo ya JKT ni salama yenye kuzingatia sheria na taratibu
za miongozo ya malezi ya vijana wanaopokelewa makambini wanalelewa vizuri
kulingana na Mila na desturi za Nchi yetu.
0 Comments