MKURUGENZI
Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA) Mhandisi
David Palangyo ameeleza hatua ambazo mamlaka imechukua ili
kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo kuunda vikundi vidogo vidogo ambavyo
vinajihusisha na ufugaji wa nyuki pamoja na kupanda miti kando ya mto Ruaha.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dodoma Mkurugenzi huyo ameeleza utekelezaji
wa majukumu ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Iringa (IRUWASA) amesema
kuwa mamlaka hiyo imeunda vikundi vya kujishughulisha na ufugaji wa nyuki
ambapo nyuki hao husaidia kupambana na maadui na vikundi vingine vinajihusisha
na upandaji wa miti kandokando ya mto Ruaha ambapo itasaidia kukabiliana
na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Amesema
kuwa mamlaka hiyo imeweza kuwafikishia wananchi huduma ya maji safi
na salama kwa asilimia 97 kwa wakazi wa manispaa ya Iringa na inatoa huduma
ndani ya masaa 23 kwa siku na hivyo basi imeweza kutimiza adhma ya serekali ya
kumtua mama ndoo kichwani.
Tumeweza kuvuka sera ya maji na ilani ya Chama Cha mapinduzi kwa kutoa huduma ya maji kwa asilimia 97 na tumeweza kumtua mama ndoo kichwani.
Hata
hivyo amesema kuwa mamlaka hiyo imekuwa na mafanikio ya kitehama ambapo ni
pamoja na kufunga mita za kisasa ambazo ni mita za malipo ya awali (pre
paid) ambazo zimeweza kuwafikia wanachi takribani 6700 kwa manispaa ya
Iringa na taasisi za kiserekali.
Pia
mamlaka hiyo imeandaa mipango mikakati ambayo itaweza kukabiliana na changamoto
zinazoikabili ikiwemo ujenzi wa chanzo kingine cha Mto Mtitu katika manispaa ya
Iringa ili kuongeza upatikanaji wa maji.
0 Comments