KATIKA kutekeleza mkakati wa kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara mtandao barani Afrika watoa huduma wa Posta wametakiwa kuwa na Sera imara ya mpango wa utekekezaji wa mahitaji ya miundombinu ya kuwezesha uchumi wa kidigital.
Akimuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakati akifungua maadhimisho ya siku ya posta Afrika ulioenda sambamba na semina kwa watoa huduma za posta Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta TCRA DKT Emanuel Manase amesema huduma za kiposta zinakuwa kwa kasi na kufungua fursa katika maeneo mbalimbali.
Dkt Manase amesema huduma za kiposta zinakuwa kwa kasi na kufungua fursa katika maeneo mbalimbali nchini.
Tanzania inakua mwenyeji wa maadhimisho haya ya siku ya Posta Duniani, kabla ya kufika katika kilele chenyewe taasisi za serikali Leo Jijini DODOMA zinajiweka katika hadhara ya Watanzania kueleza namna Shirika la Posta ambavyo limekua mgongo katika kuifungua nçhi kibiasharaWakati akiyafungua Maadhimisho hayo Jijini hapa Dkt Manase anaona kuna umuhimu wa kuwapo kwa sera madhubuti na kuimarisha ushindani wa biashara barani Afrika.
Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ni "Mwezeshaji mahiri wa biashara ya mtandao inayovuka mipaka barani Afrika"
0 Comments