MAKAMU wa Rais, Dokta Philip Mpango amewaagiza viongozi kuanzia ngazi ya mitaa hadi Mkoa kuhakikisha watoto wote waliotakiwa kuingia shule za awali, msingi na kidato cha kwanza mwaka huu, wanakwenda kuripoti shuleni.
Agizo hilo amelitoa leo January 20 Jijini Dodoma katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Angela Kairuki kwenye mkutano mkuu wa kutangaza mafanikio yaliyopatikana katika mkoa wa Dodoma kwa kipindi cha miaka miwili chini ya Serikali ya awamu ya sita.
Aidha Dokta Mpango pia amewataka wakuu wa mikoa nchini kutekeleza agizo lake la kila Mkoa kuanzisha kilimo katika maeneo ya mijini na kila mkoa kutenga maeneo na kuweka katika mipango yake kila wanapopima ardhi.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamle amesema katika kipindi Cha miaka miwili Mkoa wa Dodoma unajivunia ongezeko la bajeti ya sekretarieti ya mkoa kutoka shilingi bilioni 314.9 mwaka 2020/2021 hadi shilingi bilioni 372.06 mwaka 2022/2023.
Kwa upande wake Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda amesisitiza kuwa na mpango maalum kwa ajili ya watu waishio kijijini ambao ndio wakulima na wafugaji ili kuweza kuinua sekta ya kilimo.
0 Comments