WAZIRI wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo
amewataka wakuu wa Mikoa na Wilaya kusimamia zoezi la upandaji miti katika maeneo
yao ili kufikia lengo lililowekwa na Serikali.
Pia, amewataka viongozi
wa Majiji na Manispaa kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS) na Wakala wa Barabara Mijiji na Vijijini (TARURA) kuwa na miti ya
kutosha kando ya barabara zinazopopita katika maeneo yao ili kuhifadhi
mazingira.
Dkt. Jafo ametoa
kauli hiyo leo Januari 10, 2023 wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kando
ya barabara jijini Dodoma ikiwa ni Wiki ya Maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar.
Amesema baada ya
nchi yetu kukumbwa na ukame katika baadhi ya maeneo ni vyema sasa wananchi
wakatumia mvua hizi zinazoendelea kunyesha kupanda miti ya kutosha katika maeneo
yetu na kwenye vyanzo vya maji.
Viongozi twendeni tukasimamie Wilaya zetu kwa kupanda miti milioni 1 na laki tano kwa kila Halmashauri ili tufikie lengo la kupanda miti milioni 276 sasa jambo hili tutalifanikisha kwa kutumia mvua hizi kupanda miti, hapa nataka niwapongeze Dodoma mmeonesha mfano na ndani ya miaka mitatu mtakuwa Jiji la mfano kwa utunzaji mazingira
Akiendelea
kuzungumza na wananchi pia Waziri Jafo amewataka wataalamu wa kilimo wabainishe
aina za miti ipandwe katika maeneo gani ili kueupuka changamoto ya baadhi ya
miti kufa.
Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh Dk Selemani Jafo akipanda mti kando ya Brabara jijini Dodoma ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar |
Sanjari na hilo
pia amesisitiza kila mwananchi anayeomba kibali cha ujenzi wa nyumba ahakikishe
anakuwa na mpango wa kupanda miti angalau mitatu na kuendelea ili tuwe na miti
ya kutosha hivyo adhma ya kupambana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi
inafanikiwa.
Zoezi la
upandaji miti limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa
Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri, wanafunzi, wadau wa mazingira na
wananchi kwa ujumla.
0 Comments