KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo amewaonya viongozi wanaolalamika kuhusu maeneo wanayopewa kufanyia kazi hali ambayo inawavunja moyo wananchi ambao wanawategemea kutatua kero zao huku akisisitiza hawatakua na huruma katika kuchukua hatua kali za kisheria kwa kuwawajibisha wahusika.
Chongolo ametoa onyo hilo Leo jijini Dodoma wakati wakupokelewa kwa Wajumbe wa Secretarieti mpya ya chama cha Mapinduzi Taifa ambapo amesema wanashangaa kuona baadhi ya viongozi wakiwemo Mawaziri, wakuu wa mikoa na baadhi ya viongozi wanalalamika kutopewa ushirikiano na watumishi hali ambayo imekistua chama na kuwatathmini kwamba hawawezi majukumu wanayopewa na wajitathmini wao wenyewe kama wanatosha kwenye nafasi zao.
Mbali na kuwakemea Viongozi hao amewatangazia kiama viongozi hao ambao wanatumia muda mwingi kulalamika na kueleza kuwa kulalamika kwao kunaonesha wazi kuwa hawatoshi na kama hawawezi kufanya kazi wakae pembeni.
Changamoto kubwa tuliyokuwa nayo ndani ya chama chetu ni kuwepo kwa baadhi ya watumishi ndani ya serikali kuendelea kulalamika, unamkuta Waziri aliyepewa dhamana ya kutimiza wajibu wake, Mkuu wa Mkoa na mkuu wa Wilaya badala ya kutimiza wajibu wao bado wao wanaendekeza kulalamika.
Hii ni aibu mfano unawakuta watumishi wa serikali wanaenda kwenye vyomba vya habari wanawalalamikia watendaji waliopo chini yao kuwa hawasaidii kufanya kazi kwa kitendo hicho kinaonesha wazi kuwa hautoshi ni sawa na Katibu mkuu kuwalalamikia waliopo chini yake kuwa hawasaidii kazi je unawezaje kulalamika wakati unatakiwa kutumia mamlaka uliyo nayo
Chongolo.
Pamoja na mambo mengine Chongolo amesema kuwa Sekretarieti imeaminiwa zaidi kwa ajili ya kuhakikisha inafanya kazi kwa nia ya kuhakikisha inatatua matatizo ya watanzania na kujibu hoja.
Ndugu zangu 2019 chama kilipewa dhamani ya kushika nafasi za serikali za mitaa wajibu huo unatakiwa kusimamia ili tuendeleee kuaminiwa zaidi na zaidi ndugu zangu wajibu huo si wakukaa kilegelege, kulala wala kuzembea .
Changamoto nyingine tulitonayo kwa baadhi yetu ni baadhi ya watumishi waliopewa majukumu lakini hawajui majukumu ya nafasi tulizopewa, Mkuu wa Mkoa badala ya kutimiza wajibu wake anakaa analalamika hatupo kwenye wajibu wa kusikiliza malalamiko tuko kwenye wajibu wa kutenda, umepewa dhamana ya kutumikia unashindwa kutumikia unachelewesha kutimiza malengo huo ndio wajibu tunaonenda kuufanya na tutaufanya kwelikweli.
Wananchi wanataka miundo mbinu wananchi wanataka dawa za mifugo wanchi wanataka huduma sio maneneo, kama ni wachimbaji wadogo na wakubwa watendewe haki sawasawa kama ni wakandarasi wa ndani na nje watendewe sawasawa wasipotendewa sawasawa watatunyoshea kidole tukiruhusu wananchi watunyooshee vidole tutakuwa hatutendi sawasawa
Chongolo.
Mimi ni chongolo ila nikiwa hapa mimi ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi hivyo sitaki kuona viongozi watakaosababisha maswali mengi kwa watanzania yasiyokuwa na majibu tunataka vitendo siyo maneno
Katika hatua nyingine Chongolo amesema kuwa wiki hii wanaanza ziara mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kukagua miradi kuanzia ngazi ya shina huku akiwataka watendaji wa juu kuhakikisha wanatoa ushirikiano na watumishi wa ngazi ya chini.
Aidha Chongolo amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya kuchekeana na kufimbiana macho katika mambo ya msingi ambayo yanagusa maisha ya watu.
Kwa upande wake Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama hicho, Sophia Mjema amesema kuwa kwa nafasi aliyopewa anaenda kufanya kazi kwa mitazamo tofauti kwani kabla ya kwenda kwa wananchi lazima idara hiyo ya uelimishaji iwe sawa .Lazima mabalozi wetu wakajue wananchi wanataka nini lazima ndugu zetu tutakapokwenda kwa wananchi tutaenda mpaka ngazi za vitongoji tukajue wananchi wanataka nini
Mjema.
Amesema katika kukitangaza chama wanaCCM wanatakiwa kufanya kazi wote kwa pamoja kwani hakuna mwingine atakayekilinda chama bali ni wao.
0 Comments