SERIKALI imesema hadi ifikapo 2025 haitaagiza sukari nje ya nchi kwani tayari kutakuwa na uzalishaji wa kutosha ndani ya nchi.
Hayo yamesemwa leo Januari 10 2023 na Waziri wa Kilimo Husein Bashe wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari ambapo amesema lengo la Serikali lilikuwa ni kutoagiza sukari nje ya nchi ifikapo 2030.
Malengo ya nchi ni hadi ifikapo 2030 import (uingizaji) wa sukari iwe zero, lakini kwa mikakati tuliyoiweka nawahakikisha tutakuwa na import ya sukari zero by 2025.
Tumegundua tatizo liko wapi, maana mwaka jana zilimwagwa tani za miwa zipatazo laki tatu kisa wakati wa kuvuna miwa inayovunwa kwa mtindo wa ushirika kuna baadhi ya wakulima ambao hawaishi maeneo ya ushirika ulipo mashamba yao hayakuvunwa, lakini mwaka huu zimemwagwa Tani 8000 tu, kwa hiyo tumegindua hilo lilikuwa linatupa hasara.
Waziri huyo amesema Wizara yake itahakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030 inapunguza kwa kiasi kikubwa kuagiza bidhaa nyingine kama mafuta ya kula, ngano, mchele zinazoagizwa nje ya nchi .
Sanjari na hayo amesema mikakati mingine katika Wizara hiyo ni kuboresha eneo la uzalishaji wa mbegu bora ili kutosheleza mahitaji ya nchi.
Amesema hatua hiyo itaiwezesha nchi kuzalisha kwa tija na hivyo kuifanya nchi kujitosheleza kwa chakula kutokana na uzalishaji wenye tija utakaotokana na mbegu bora.
Hata hivyo amesema delta ya Kilimo inachangia katika Pato la Taifa kwa asilimia 26.1 huku akisema sekta hiyo inachangia katika malighafi za viwandani kwa asilimia 65.
0 Comments