Mkurugenzi
wa Mipango kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Mosses Dule amewashauri
wanataaluma waliosoma katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini
kukutana,kuzungumza na kuanisha mahitaji yanayohitajika chuoni humo ili
kuyafanyia kazi.
Amezungumza
haya leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada
kuhitimisha kongamano la Kitaaluma lililofanyika katika chuo hicho.
Hawa wenzetu ambao wamesoma hapa wanarejesha nini kwenye hiki chuo?,
Dule
Familia ikikusomesha tunatarajia kuwe na mrejesho. Sasa ule mrejesho umekuwa na changamoto. Kwa hiyo sasa wakutane,wazungumze ,waainishe ni mahitaji gani yanahitajika ambayo yanakwaza spidi ya maendeleo ya chuo. Kama ni kushauri washauri kama ni kutoa msaada wa vitu, hela waweze kufanya hivyo.
Aidha,
amekipongeza chuo hicho kwa kufanya kazi ya kuboresha programu mbalimbali
ambazo zimesaidia kuzalisha wanataaluma wenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi
katika maeneo yao ya kazi.
Sisi kama Wizara tutaendelea kuwasaidia kuweza kutekeleza mipango yao . Wana dira ambayo wanaitekeleza tunahitaji kuwezesha kufika kule wanapotaka kufika.
Wakati
huo huo ,amesema nia yao ni kuhakikisha wanaimarisha vituo ambavyo vipo kwenye
chuo kwa baadhi mikoa ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi .
Utaona wanafunzi unaowaona hapa umri wao ni mdogo sana. Sasa hosteli hamna sasa tunataka kuwalinda hawa . Ndio maana katika kipindi cha kama miaka mitano kila mwaka tunawatengea hela si chini ya bilioni 5 kwaajili ya kuimarisha miundombinu ya kujifunza na kufundishia.
Chuo hicho kimewakutanisha wanataaluma hao waliosoma chuoni humo ili waweze kubadilisha uzoefu, kuzungumzia chuo kinafanya nini ,wamepata kitu gani wakati wanasoma na kile walicho kipata kimesaidia nini kwenye utejekezaji wa majukumu yao baada ya kuhitimu.
0 Comments