NAIBU
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Jenifa Omolo amewataka wahitimu wa Chuo
cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kuendelea kuwa chachu ya kujifunza ili
kuongeza maarifa ,ujuzi na ubunifu unaohitajika katika kuboresha utendaji wao
wa kazi.
Ameyasema
haya leo katika Mahafali ya 36 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dodoma,
ambapo amesema kwa wale watakao endelea na masomo ya ngazi ya juu wanapaswa
kuendelea kujifunza kwa bidii ili kupata maarifa na ujuzi utakao wawezesha
kuhimili mazingira ya ulimwengu wa kisasa wa kazi ya maendeleo ya uchumi ya
familia zao na taifa kwa ujumla.
Nawapongeza wahadhiri wa chuo kwa kushiriki katika kuwapa maarifa na ujuzi wahitimu hawa. Nyie ndio mlikuwa wapishi wa chakula ambacho kinapakuliwa leo tayari kwa kutumika katika soko la ajira. Soko huru lenye mahitaji mbalimbali kwa sasa ikiwemo soko la kidigitali
Aidha,
amewapongeza wazazi, walezi na wafadhili mbalimbali waliogharamia masomo ya
wahitimu hao kwani uwekezaji huo uliofanyika umesaidia kuongeza mtaji wa watu
katika taifa.
Na hivyo kuongeza uwezo wa kuzalisha, kukuza uchumi na kuboresha hali ya maisha ya wananchi wetu.
Kwa
upande wa Mkuu wa chuo hicho Profesa Hozen Mayaya amesema chuo kimeendelea
kufundisha kwa kutumia mitaala inayokidhi matakwa ya soko na inayozingatia
umahiri.
Mitaala ya chuo huwapatia wahitimu wa elimu ya sekondari pamoja na vyuo vya kati fursa ya kujiendeleza katika fani mbalimbali za mipango ya maendeleo kuanzia ngazi ya astashahada hadi ngazi ya uzamili.
Prof. Mayaya
0 Comments