📌RHODA SIMBA
WADAU
mbalimbali wameshiriki kwenye SEPESHA RUSHWA MARATHON na imenoga akiwemo mzee
mwenye umri wa miaka 74 kushiriki.
Lengo la mbio hizi ni kuongeza uelewa juu ya Madhara ya Rushwa pamoja na kukusanya fedha kwaajili ya mradi wa BADILI TABIA,
Mbio hizo zimeandaliwa na asasi ya kiraia ya Anti-Corruption Voices Foundation [ACVF] zilizohusisha wadau mbalimbali ambapo walishiriki katika mbio za kilomita 3, 5, 10 na 21 katika mitaa na viunga vya jiji la Dodoma kutokea uwanja wa Jamhuri.
Mbio hizi ziliishia uwanja wa Jamhuri ambako washindi na washiriki wote walipewa zawadi na medali kadiri ya umbali waliokimbia.
Moja kati ya matukio yaliyowavutia wengi ni ushiriki wa Mzee Sakhoo ambaye alitimiza umri wa miaka 74.
Sachoo alisema amekuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kila siku ndio sababu kuendelea kuwa na afya njema.
Katibu Mtendaji wa ACVF, Kubega Dominiko alisema mashindano hayo yamekuwa na ubora wa hali ya juu.
Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma kutoka
Takukuru, Mhandisi Joseph Mwaiswelo aliwashukuru wale wote walioshiriki mbio
hizo na kuwasisitiza kuendela kutoa elimu ya Madhara ya Rushwa katika jamii.
0 Comments