📌 MWANDISHI WETU
RAISI wa UTPC, Mkurugenzi wa UTPC na Wenyeviti wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania wameshiriki katika Kongamano la Kitaifa la Maendeleo ya Sekta ya Habari lililoandaliwa na Idara ya Habari Maelezo leo tarehe 17/12/2022
Kongamano hili pia linawaleta pamoja wadau wengine wa Habari wakiwemo Wahadhiri, Maafisa Habari wa Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, Maafisa habari wa Sekta binafsi, Wawakilishi kutoka mashirika ya kimataifa yaliyopo nchini na Wanafunzi wa Elimu ya juu wa Sekta ya Habari
Mbali na mambo mengine kutakuwa na uwasilishaji wa Mada mbalimbali zinazohusu sekta ya habari.
0 Comments