MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Mary Chatanda amewaasa wanawake wa Umoja huo kuacha Makundi na washiriki katika kukijenga Chama Cha mapinduzi (CCM)
Kadhalika amewataka wanawake kushiriki katika mapambano dhidi ya ukatili ili kuwasaidia wanawake na watoto.
Ameyasema hayo Leo Disemba 9 2022 jijini Dodoma kwenye kongamano maalum la kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuchagúliwa kuwa mwenyekiti wa sita wa CCM Taifa.
UWT tunampongeza sana Rais kwa kuongoza CCM na kuhakikisha serikali inasimamia usawa wa jinsia na tunaona wanawake wengi wenye uwezo wamepata fursa katika ngazi za maamuzi na juhudi zake zimepelekea kufikia usawa wa kijinsia kwa kutekeleza kuanzia ngazi ya siasa
Amekuwa mdau mkubwa wa usawa wa kijinsia katika uongozi wake, tunajivunia kuwa na Rais wa kwanza mwanamke tangu tupate uhuru mwaka 1961
Chatanda.
Amesema wao kama UWT watahakikisha kuwa watashiriki kwenye mapambano dhidi ya ukatili na watakuwa mstari wa mbele kupambana na dhihaka na kutokumkwamisha Raisi kwa kazi anazozifanya.
Naye mbunge wa viti maalum Mkoa wa Dodoma Fatuma Taufiq amesema anaungana na wanawake wenzake kumpongeza Rais Kwa kuchaguliwa katika nafasi hiyo na kwa kujitoa kwake kwa kuwaletea watanzania maendeleo.
Leo Wanawake tumekuja hapa tuna jambo letu kwanza kumpongeza Rais kwa kura za kishindo sisi wanawake kwakweli tuna kila sababu ya kumpongeza kwani ametupatia maendeleo makubwa kwa mkoa wa Dodoma
Toufiq
Akizungumza kwa niaba ya mawaziri wanawake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Anjela Kairuki amesema Rais Samia amekuwa kiongozi mahiri na mchapakazi katika utendaji wake wa kazi.
Mafanikio ya kazi yakeyanajiuza, uongozi mahiri, uchapakazi kusema ukweli amekuwa akisimamia anachokiamini ametekeleza miradi ya maendeleo tumeona ameimarisha huduma za kijamii. Lakini pia ameimarisha miundo mbinu ujenzi wa madaraja hospitali, mapambano dhidi ya rushwa pia amepambana kuimarisha uchumi na sera, mapato na matumizi .
Kairuki
Naye Mwenyekiti UWT Dodoma Neema Majure amesema zaidi ya wanawake 4000 wamekusanyika katika tukio hilo.
Hatuwezi kunyamaza kwa mambo anayoyafanya tumeona tukutane hapa tuweze kumpongeza ametuheshimisha wanawake kwa ushindi .
Majure
Hata hivyo Dkt. Getrude Mongela ambaye ni Spika wa Bunge la Afrika Mashariki naye amesema nchi ya Tanzania kwa Afrika imebarikiwa kumpata mwanamke Rais lakini pia kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Enzi zile ukiteuliwa kuwa Waziri unasali sana usikosee ukikosea wanawake wenzio wanakucheka wanasema mnaona wanawake tutamsaidia Rais Samia azibe mwanya wa wanawake hatutaki kunyooshewa vidole kwamba wanawake mnawaona hawawezi kufanya peke yake ni sisi sehemu zote tutamshika mkono .
Mongela.
0 Comments