📌MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana amepokea tuzo ya Kimataifa International Iconic Awards ya nchini India iliyotolewa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan .
Tuzo hiyo imekabidhiwa Disemba 11,2022 Jijini Dodoma na Uongozi wa Miss Jungle International na Bega kwa Bega na Mama (BBMF) .Kutolewa kwa tuzo hiyo kwa Rais kunatokana na Programu ya Tanzania – The Royal Tour aliyoifanya iliyoitambulisha nchi kitaifa na kimataifa kutokana na vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar ambayo imesaidia kuvutia watalii wengi.
0 Comments