MILIONI 960 ZILIZOPANGWA KUFANYIA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA UHURU KUELEKEZWA KWENYE UJENZI WA SHULE.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

RAIS Samia Suluhu Hassan ameamuru fedha zote kiasi cha shilingi milioni 960 kilichopangwa na ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanzania, zipelekwe ofisi ya Rais Tamisemi kwa ajili ya ujenzi wa mabweni nane katika shule za watu wenye mahitaji maalum.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu George Simbawene wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya Uhuru yanayoadhimshwa hapa nchini Desemba 9, ya kila mwaka.

Aidha Simbachawene amesema, maadhimisho hayo kwa mwaka huu hayataadhimishwa Kitaifa isipokuwa yataaadhimishwa kila Wilaya kwa kufanya midahalo na makongamano.

Mwaka huu hakutakuwa na gwaride wala shughuli ya Kitaifa na badala yake maadhimisho yafanyika kila wilaya na fedha zote zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya maadhimisho hayo zipelekwe ofisi ya Rais Tamisemi ili zikajenge mabweni nane katika shule za msingi za wenye mahitaji maalum

Simbachawene

Simbachawene ameagiza wakati maadhimisho hayo, ofisi zote za serikali zipambwe kwa mampambo ya bendera ya Taifa na picha Rais huku akitaka kuwe na majadiliano ya kina katika makongamano na midahalo hiyo.

Aidha Waziri huyo amesema shule hizo zimesharatibiwa na Ofisi ya Rais Tamisemi huku akizitaja shule hizo kuwa ni Buhangija ya mkoani Shinyanga, Darajani Mkoani Singida, Songambele Manyara, Mtamba Tanga, Nsazi Rukwa, Idofi Njombe na Longido mkoani Manyara

Simbachawene amesema hiyo ni dhamira ya dhati ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha anatengeneza mazingira mazuri ya kujifunzia kwa watu wenye mahitaji maalum.

 

 

Post a Comment

0 Comments