KLABU YA WANDISHI WA HABARI DODOMA YAFANYA MKUTANO MKUU MAALUM

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa ahabari Mkoa wa Dodoma (Mussa Yusuph) akifungua Mkutano Mkuu Maalum , uliofanyika leo Disemba 19 katika Ukumbi wa Kinyaiya Roma Complex Jijini Dodoma (Kushoto ni Katibu Mkuu wa Klabu, Ben Bago na Kushoto ni Mhazini Jasmine Shamwepu)


📌MWANDISHI WETU

KLABU ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) imefanya Mkutano Mkuu Maalum leo Disemba 19 katika Ukumbi wa Kinyaiya Roma Complex Jijini Dodoma

Lengo kubwa la Mkutano huu ni kufanya Maboresho ya Katiba ya Klabu ikiwa ni miongoni mwa maazimio ya Mkutano Mkuu wa UTPC uliofanyika katika Ukumbi wa Millenium 2 Kisenga Hall tarehe 6 Jijini Dar es Salaam pamoja na kukubaliana kuandaa Muongozo maalum wa Utatuzi wa Migogoro katika Klabu

Maazimio haya yatasaidia kuendana na kasi ya kuitoa UTPC kutoka kwenye ubora kwenda kwenye ubora zaidi (Moving UTPC from Good to great)

Pamoja na mambo mengine, wanachama wamepokea Taarifa ya Utekelezaji wa klabu na Taarifa ya Fedha





Wanachama wakichangia Mada katika Mkutano Mkuu 




Post a Comment

0 Comments