UTPC na Jamii Forums wameingia katika
Ushirikiano wa Kimkakati kwa lengo la kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari
Nchini katika kuandaa Habari za Kiuchunguzi (IJ) na zenye Maslahi ya Umma (PIJ)
ili kuchochea Uwajibikaji na utawala bora
Pia, Waandishi watajengewa uwezo kuhusu Usalama wa Kidijitali, matumizi sahihi na bora ya Vifaa na Mifumo ya Kidijitali na namna bora ya kutumia Uwanja wa Kidijitali kuendeleza kazi zao
Aidha, Mkurugenzi wa JamiiForums amesema litaanzishwa shindano la #StoriesOfChange litakalowalenga waandishi wa habari na washindi watatuzwa baada ya mchujo
Ushirikiano huu ni miaka 2, utaanza rasmi Januari 2023 na unaweza kuhuishwa baada ya kufanya tathmini
0 Comments