HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi imemteua Dkt. Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa chama hicho kuwa mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho kwa kipindi cha mwaka 2022 /2027.
Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka wakati akiongea na waandishi wa habari kuelekea kwenye Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho Disemba 7 jijini Dodoma.
Dkt. Samia Suluhu Hassan atapelekwa kwenye mkutano mkuu kesho kwaajili ya kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu ili aweze kuchagúliwa kuwa mwenyekiti wa çhama kwa muhula huu ambao nimeuainisha, Halmashauri kuu pamoja na mambo mengine imepokea pendekezo na kuridhia ndugu Abdulhamani Kinana kuwa Makamu mwenyekiti ambaye anaenda kukamilisha hatamu yake ya uongozi lakini Halmashauri kuu imeweza kupendekeza tena.
Shaka
Aidha, Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi imepokea pendekezo na kuridhia Dkt. Hussein Ally Mwinyi kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa upande wa Tanzania Zanzibar.
Sasa hivi nafasi hiyo imeshiikiliwa na Dkt Ally Mohamed Shein ambaye anakwenda kukamilisha hatamu yake ya uongozi ambapo alikuwa Rais wa Zanzibar Mstaafu wa awamu ya saba na sasa hivi ndio Makamu mwenyekiti anaekwenda kukamilisha muda wake
Shaka
Kadhalika Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi pamoja na mambo mengine imepokea mapendekezo ya kuyajadili na kuyachakata na hatimaye kufanya uteuzi wa wanachama ambao wameomba ridhaa ya chama wateuliwe kuwa wagombea wa nafasi ya halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi, nafasi ambayo inataka watu 15 Tanzania Bara na watu 15 Tanzania Zanzibar
Tanzania Bara halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi cha CCM imewateua wanachama 251 kuwa wagombea wa nafasi za ujumbe wa Halmashauri ya Taifa hao nao watapigiwa kura siku ya kesho, kadhalika kwa upande wa Zanzibar wanachama 123 watasimama kugombea nafasi za ujumbe wa halmashauri ya Taifa ya CCM ambao wote wataungana kuomba kura siku ya kesho
Shaka
Hata hivyo amesema kuwa Uchaguzi huo unaofanyika kesho umezingatia usawa wa kijinsia ambapo chama kimetoa fursa kwa pande zote mbili kwani jumla ya wanachama 172 wanaume wameteuliwa kugombea nafasi za ujumbe ya Halmashauri kuu Taifa Tanzania Bara huku jumla ya wanachama 79 wanawake wakiteuliwa kugombea katika nafasi hizo
0 Comments