📌NA MWANDISHI MAALUMU
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesisitiza suala la maadili shuleni na kukemea tabia zisizofaa kwa baadhi ya walimu.
Profesa Mkenda ametoa msisitizo huo jijini Dar es Salaam wakati wa mahafali ya kidato cha nne ya shule 11 za kiislamu ambapo amesema hatua za zitachuliwa kwa yeyote atakaepotoka kimaadili.
Tunakoelekea tutakuwa wakali zaidi, natoa tahadhari kwa walimu na wenye shule kusimamia kwa karibu malezi ya vijana
Prof.Mkenda
Alisema walimu na wamiliki wa shule wana wajibu huo hivyo wa malezi hivyo kinachotakiwa ni kuzingatia jukumu hilo ili wanafunzi waweze kupata malezi ambayo wazazi wanatarajia wqkiwq shule.
Katika hatua nyingine amezishukuru shule binafsi zikiwemo za kidini kwa kuendelea kutoa elimu bora jambo linalosaidia kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu bora nchini kote.
Lakini pia alisema lipo suala la mitaala pamoja na masomo ya dini, hivyo kama alivyoombwa amelipokea na Wizara italishughulikia.
Awali Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, ambaye ni mlezi wa shule za kiislam Dar es Salaam, Alhad Mussa aliwausia wanafunzi waliomaliza waendelee kuwa na maadili mema.
Elimu bila maadili haina maana mbele ya taifa linalowategemea kama viongozi wa Kesho.SheikhAlhad Mussa
Alisema taifa likikosa maadili ni sawa na kusema hilo ni taifa mfu.
Wanafunzi waliohitimu waliotoka sekondari zikiwemo Ilala Islamic, Qiblatain, Dar es Salaam Islamic, Kunduchi Girls Islamic, Al-haramain, Ununio Boys Islamic, Muzdalifa na Temeke Islamic.
0 Comments