SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya Watu Duniani (UNFPA) limeahidi
kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutoa elimu na kuhakikisha wananchi
wanatambua matumizi sahihi ya matokeo ya Sensa ya watu na makazi iliyofanyika
Agosti 23 mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dodoma mara baada ya kufanya mazungumzo na
mwakilishi mkazi wa UNFPA Wilfred Ochuan ambaye anamaliza muda wake hapa
nchini, Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anne Makinda amesema matokeo ya Sensa
yanatakiwa yalete tija kwa wananchi katika kufikishiwa shughuli za maendeleo na
huduma za kijamii.
Katika shirika lililotusaidia sana kufanikisha sensa yetu hii ni UNFPA kwasababu kimataifa wao ndio wanao simamia mambo ya idadi ya watu
Makinda.
Amesema
walikuwa wanasaidia kwenye mambo ya ufundi, vifaa na kuwashirikisha na mataifa
mengine ikiwemo kupata vishikwambi 600 kutoka South Korea, 200 kutoka UN WOMEN
na China.
Huyu Wilfred Ochuan ameteuliwa kwenda Ghana kuwa mwakilishi wa idadi ya watu hivyo alikuja kutuaga na kuaga wafanyakazi wa hapa
Makinda.
Yeye ameahidi kwamba wataendelea kutusaidia ili watu waweze kujua matumizi ya takwimu sasa hatuna mila sana ya kutumia takwimu lakini kwa sasa tunataka hilo liweze kuonekana kabisa
Pia
amesema watatumia takwimu hizo kufanya mipango yao, ufatiliaji wa maendeleo
mbalimbali ili ziweze kutumika kwenye bajeti ya serikali na waliahidi Euro laki
2.
Tujaribu kutafuta mbinu zote watanzania tuanze kutumia hizi sensa, kwani sensa zinagharama sana kwahiyo huwezi kufanya kitu kwa gharama halafu badae unakiacha tu
Kwa
upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt Albina Chuwa amesema Tanzania ina watu
wakarimu kama ilivyo kwa wananchi wa nchi ya Ghana ambao nao pia siku zote
wameonekana wakarimu hivyo tuna imani utakwenda kutusaidia kupeleka picha ya
nchi ya Tanzania ilivyo .
Bila shaka tunaimani utachukua yale yote mazuri yaliyopo Tanzania kwani hata Rais wetu wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan amekuwa akiishangaza dunia kwa mambo makubwa anayoendelea kuyafanya
Chuwa
amesema katika suala zima la takwimu nchi ya Tanzania imekuwa bingwa na imeonekana
ni nchi inayoendelea kukua kiuchumi kwa takwimu za Afrika .
Mafanikio hayo yote yamekuja kutokana na kuwa na mawasiliano na uwazi kwani ndio kitu kikubwa kwetu na pia tunajivunia kuwa na mtu kama mama Anna Makinda ambaye ndio aliyekuwa kamisaa wa sensa Tanzania bara
Akizungumza Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa UNFPA anayemaliza muda wake Wilfred Ochang aliishukuru serikali kwa kuweza kushiriki katika zoezi zima la sensa kwani ameweza kujifunza mambo mengi mazuri na makubwa juu ya masuala yote ya sensa.
Nawahakikishia kuwa naenda kupeleka mazuri yote yaliyomo na niliyoyapata katika nchi ya Tanzania, na hongereni kwa kuweza kufanikisha zoezi zima la sensa ya watu na makazi
Kwa nchi ya Ghana tunakwenda kufanya sensa ya kidigitali mwezi mei 2023 japokuwa tumechelewa lakini tunaendelea kujifunza na hakika nitakwenda kupata uhakiki baada ya kukamilika kwa zoezi zima la sensa ya kidigitali hivyo naomba ushirikiano kutoka kwenu
0 Comments