📌WAF- DOM
SERIKALI
Kupitia Wizara ya afya inaelekea kukidhi kiu ya Wananchi wa Mkoa wa
Iringa kwa kupeleka kusoma jumla ya madaktari 12 watakaotoa huduma
katika fani mbalimbali katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel leo Novemba
8, 2021 katika kikao cha bunge, Jijini Dodoma wakati akijibu swali la
Mhe. Nancy Hassan Nyalusi Mbunge wa viti maalumu.
Amesema,
Katika kuongeza idadi ya madaktari bingwa, Wizara imepeleka kusoma
jumla ya madaktari kumi na mbili (12) kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
Iringa ambao watasaidia kuboresha huduma kwa wananchi wa Mkoa huo.
Akifafanua
hilo Dkt. Mollel amesema, madaktari hao ni pamoja na; madaktari wawili
wanasomea kinywa, sikio na koo, madaktari bingwa wa mifupa wawili,
daktari wa magonjwa ya dharura mmoja, madaktari bingwa wa Watoto wawili,
madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani wawili, daktari bingwa wa meno
mmoja, daktari bingwa wa usingizi mmoja na daktari bingwa mbobezi wa
masuala ya Watoto mmoja.
Aidha,
Dkt. Mollel amesema, hadi sasa Hospitali hiyo ina jumla ya madaktari
bingwa kumi na moja 11, madaktari bingwa wa afya ya akina mama na uzazi
wanne, madaktari bingwa wa upasuaji wawili, daktari bingwa wa magonjwa
ya ndani mmoja, daktari bingwa wa Watoto wawili, daktari bingwa wa
macho mmoja na daktari bingwa wa mionzi mmoja.
0 Comments