CHAMA cha Mapinduzi CCM kimefuta na kusimamisha baadhi ya chaguzi mbalimbali zinazoendelea ndani ya Chama hicho katika Mikoa ya Simiyu, Mbeya na Arusha kwa muda usiojulikana kutokana na kubaini kuwepo kwa tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wagombea .
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa chama hicho Daniel Chongolo amesema, uchunguzi wa kina unaendelea kufanyika kwenye maeneo husika ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa watakao bainika kujihusisha na vitendo hivyo.
Mikoa ambayo tumefanya uamuzi ni pamoja na kufuta uchaguzi wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Simiyu, pia tumesimamisha uchaguzi wa Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya kwa sababu ya tuhuma mbalimbali zikiwemo za rushwa ambako nako tunafanya uchunguzi wa kina tukikamilisha tutatoa taarifa ya uamuzi wa chama
Vile vile tumesimamisha uchaguzi wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Arusha kwa sababu hiyo hiyo ya rushwa na tukikamilisha uchunguzi tutatoa taarifa za uamuzi wa chama ili kuruhusu mchakato wa uchaguzi kuendelea.
Chongolo
Katibu pia amezungumzia kuhusu tukio la wanachama kuondoka na boksi la kura katika uchaguzi uliofanywa jana mjini Magharibi Zanzibar.
Taarifa zilieleza kuwa watu hao walienda na boksi hilo kwenye chumba kilichokuwa kimeandaliwa kwa ajili ya kuhesabia kura .Sasa tunataka kuangalia uchukuaji wa boksi hilo ulilenga kuhesabu kura au ulikuwa una lengo lingine, tutafuatilia tukijiridhisha tutachukua uamuzi ukiwemo kuufuta uchaguzi na kurudiwa upya ili kutenda haki .
0 Comments