📌RHODA SIMBA
KATIKA
kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi wa wahandisi nchini,Bodi ya
wahandisi (ERB) imesema imeweka mipango ya kukuza na kuimarisha weledi
wa sekta ikiwemo na kupambana na vitendo vya rushwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Novemba 10 jijini Dodoma wakati akielezea
utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa
fedha 2022/2023 Msajili wa Bodi ya wahandisi Bernad Kavishe amesema
Bodi itaweka maslahi ya Umma mbele ikiwemo na kuzingatia maadili.
"Wahandisi
pia lazima wadhibitiwe wawe na nidhamu na maadili mema wawe na uadilifu
na kwa kifupi wahandisi tunaweka maslahi ya Umma mbele na maslah yetu
binafsi nyuma na ndio maana tunachukua kiapo kuapa kuweka maslahi ya
Umma mbele,
" Bodi ipo
mstari wa mbele katika kupambana na rushwa manake rushwa ni adui wa
uhai siyo tu adui wa haki lakini malengo mahususi ya bodi ni kuimarisha
na kuhakikisha udhibiti wa kazi za wahandisi na taaluma ya wahandisi
kwasababu uhandisi hauishii shuleni uhandisi ni tunahakikisha mpaka mtu
ana staafu" amesema Mhandisi Kavishe
Aidha
Mhandisi Kavishe ametoa wito kwa watu wenye miradi kuacha kutumia
wahandisi ambao hawajasajiliwa na bodi hiyo ili kuondokana na
malalamiko pale wanapoharibiwa kazi zao.
Kinyume cha sheria kabisa kupata huduma za kihandisi nje na watu ambao hawajadhibitishwa na bodi mbalimbali za kitaaluma, ile leseni tunayokabidhi ile ndio kielelezo ambacho serikali imeipitisha kwamba huyu mtu kapata elimu sahihi hawana mashaka nae na ujuzi wake upo haiMhandisi Kavishe.
Nae
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali imewekeza
fedha nyingi kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo barabara
majengo na tayari imezalisha wahandisi zaidi ya elfu 33 na endapo miradi
ikiharibiwa ERB inahusika.
"Kuna
kazi kubwa inafanyika na miradi mingi ndani ya nchi yetu ambayo
inategemea ushauri wa wahandisi hawa na nichukue nafasi hii kuwapongeza
mpaka sasa nchi yetu imezalisha wahandisi zaidi ya elfu 33 na 26 wapo
sokoni wanafanya kazi, ikumbukwe kuwa tulipokuwa tunapata uhuru mwaka
1961 tulikua na wahandisi wawili tuu leo tunazungumzia hawa walio kazini
na vijana bado wapo vyuoni wanasoma wanaendelea kuzalishwa" amesema
Msigwa
0 Comments