WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amezindua bodi ya wakurugenzi ya Pamba huku akiwataka wakurugenzi hao kwenda kusimamia vyema kilimo cha pamba na uzalishaji wa zao hilo bila kusahau matumizi ya teknolojia.
Ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo ambapo pia ameitaka bodi kwenda sambamba na kasi ya Rais Samia Suluhu Hassan ili kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo na kuchangia uchumi wa nchi.
Amesema ni aibu kuona uzalishaji wa pamba unasuasua wakati ukweli ni kwamba nchi ya Tanzania ina eneo kubwa ambayo inatumika kwa kilimo cha pamba.
Nendeni mkalete mabadiliko kwani wote mliochaguliwa katika bodi hii mnatosha na ndio maana leo mko hapa tunataka kuona mabadiliko katika tasnia ya Pamba
Bashe.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Marco Ngatunga amesema wanakwenda kumaliza changamoto zote zilizokuwa zikiikabili zao la pamba kwa kuhakikisha matumizi ya Teknolojia yanazingatiwa ili kuweza kufikia kuzalisha tani Milioni 1
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi huyo amesema wanakwenda kusimamia matumizi ya teknolojia ili kuongeza uzalishaji wa pamba wenye tija.
Aidha Ngatunga amesema kabla ya kuanzishwa kwa bodi hiyo changamoto nyingine ilikuwa ni kukosekana kwa utoaji wa huduma za ugani kwa wakulima na matumizi madogo ya dhana bora za kilimo.
Tunakwenda kufanya kazi kama tulivyoaminiwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kuanzisha kampeni ya hamasa kwa wakulima kuanza kutumia vipimo sahihi vya upandaji bila kusahau wakulima kuzingatia kanuni 10 za upandaji wa zao la pamba ili tuweze kufikia malengo ya kuzalisha Tani Milioni 1 ifikapo mwaka 2025 ambalo ndio lengo la Serikali kwenye tasnia ya pamba
Ngatunga.
Akizungumzia uzalishaji wa pamba kwa mwaka huu amebainisha kuwa mwaka huu wanakwenda kuzalisha Tani 180,000 kutokana na hali ya hewa na mvua kuwa chache jua kuwa kali na kumepelekea baadhi ya maeneo pamba kutotoka chini na hata iliyotoka haikupata maji ya kutosha.
Bodi tunakwenda kuhakikisha kiwango cha juu cha uzalishaji kinapatikana ambacho tani laki 3076,000 Juhudi zikiwepo tija itaonekana kwani eneo wanalolima ni zaidi ya hekali Milioni 1 tija ikiongezeka na uzalishaji utaongezeka
Ngatunga
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya pamba Christopher Gahuma, amemuhakikishia waziri Bashe kuwa Bodi inakwenda kufanya kazi kwa ubunifu na kwa umakini wa hali ya juu katika kuhakikisha na kuendeleza kilimo cha pamba pamoja na upatikanaji wa masoko.
0 Comments