VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA KUHAMASISHA CHANJO YA UVIKO 19

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

VIONGOZI wa dini mbalimbali wameaswa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na ugonjwa wa Uviko 19 ikiwemo kuhamasisha Jamii ili iweze kupata Chanjo ya ugonjwa huo.

Akizungumza Jijini Dodoma katika kikao kilichowakutanisha viongozi wa dini mbalimbali, viongozi wa kimila pamoja na wadau, Mkurugenzi wa huduma za Afya wa Kanisa kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Dk Paul Zebadia Mbando kutoka Makao Makuu ya KKKT Arusha.

Amesema viongozi wa dini wana wajibu mkubwa wa kutoa Elimu kwa waumini wao kuhusiana na Chanjo ya Uviko 19 hivyo kila mmoja ana wajibu wa kufanya katika kutoa Elimu sahihi kwa waumini na taifa kwa ujumla.

Aidha amesema ili kuinusuru Jamii katika Majanga ikiwemo la Uviko 19 viongozi wa dini wana wajibu wa kutoa Elimu kwa wafuasi wao na kuwaondoa katika maswali magumu kuhusu Usalama wa Chanjo hiyo.

Kwa upande wake Askofu Amon Kinyunyu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Dodoma ambaye amemwakilisha Mkuu wa Kanisa la kilutheri Tanzania Askofu Dk Shoo,amesema mkutano huo utatoa njia sahihi ya namna gani wanaweza kuwaelimisha watu walio nyuma yao wanaondokane na Imani potofu kuhusu Uviko 19.

Chanjo ya Uviko 19 kama zilivyo chanjo zingine ni salama na muhimu kwa jamii, hivyo ni vyema jamii ikazingatia ushauri wa wataalamu wa Afya sambamba na kupata chanjo hiyo

Askofu Amon 

Kwa Upande wake Shekh wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya viongozi wa dini mbalimbali Mohamed Kadidi amesema viongozi wa dini wana wajibu wa kuendelea kushirikiana na viongozi wa kimila, wataalamu wa Afya na serikali katika mapambano dhidi ya Uviko 19 hivyo wajibu wao mkubwa ni kuendelea kuhamasisha jamii wapate chanjo hiyo kwani ni salama.

Naye kiongozi wa kimila jamii ya kimasai kutoka Wilaya ya Longido Thomas Ngolopa ameziomba taasisi za kidini kwa kushirikiana na serikali kufanya jitihada kubwa kupeleka Elimu ya Chanjo ya Uviko 19 kwa jamii ya kifugaji kwani uelewa kuhusu chanjo hiyo bado ni mdogo.

Wajibu wa viongozi wa dini wakishirikiana na madiwani na viongozi mbalimbali kufikisha Elimu kwa jamii ya kifugaji na kuondoa imani potofu kuwa chanjo ya Uviko 19 inasababisha vifo imani ambayo siyo ya kweli

Mkutano huo umewakutanisha viongozi wa dini mbalimbali, viongozi wa kimila na wadau kutoka mikoa Saba nchini ikiwemo Dodoma, Tanga, Morogoro, Manyara, Arusha, Singida, na Kilimanjaro.

 


Post a Comment

0 Comments