KATIKA kutekeleza majukumu ya Wakala wa barabara Vijijini na Mijini (TARURA) hadi kufikia Mwezi Juni 2022 jumla ya Shilingi bilion 673.3 zilipokelewa ili kutengeneza barabara kwa kiwango cha lami na kukarabatiwa ikiwa ni asilimia 93 ya bajeti iliyotengwa ambapo utekelezaji wake kwa sasa umefikia asilimia 81.
Akitoa Taarifa ya utekelezaji na mwelekeo wake kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma, mtendaji mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seif amesema kuwa Jumla ya km 22,202.84 zimefanyiwa matengenezo ya kawaida, km 275.85 zimejengwa kwa kiwango cha lami, km 11,120.09 zimejengwa kwa kiwango cha changarawe na jumla ya madaraja 596 yamejengwa/yamekarabatiwa.
Mwaka wa fedha 2021/22 ulikuwa mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wetu wa pili ambapo bajeti ya TARURA iliongezwa kwa takribani mara tatu na kufikia Shilingi bilioni 722 kwa fedha za ndani
Hadi kufikia Mwezi Juni 2022 jumla ya Shilingi bilion 673.3 zilipokelewa ikiwa ni asilimia 93 ya bajeti iliyotengwa na utekelezaji umefikia asilimia 81, Jumla ya km 22,202.84 zimefanyiwa matengenezo ya kawaida, km 275.85 zimejengwa kwa kiwango cha lami, km 11,120.09 zimejengwa kwa kiwango cha changarawe na jumla ya madaraja 596 yamejengwa/yamekarabatiwa
Mwaka wa fedha 2022/23 ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa pili ambapo TARURA imetengewa bajeti ya jumla ya Shilingi bilioni 838.16 ambapo kati ya hizo Shilingi bilioni 776.63 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 61.53 ni fedha za nje
Lengo kwa mwaka huu wa fedha ni kufanya matengenezo ya kawaida km 21,595.72, kujenga/kukarabati km 422.07 kwa kiwango cha lami, kujenga/kukarabati km 11,074.56 kwa kiwango cha changarawe na kujenga/kukarabati madaraja 269
Alisema kuwa katika utekelezaji wa bajeti ya Mwaka 2022/23 jumla ya zabuni 1,706 zenye thamani ya Shilingi bilioni 621.66 zimepangwa kutangazwa, awamu ya kwanza ilitengwa asilimia 60 ya bajeti sawa na zabuni 1,085 zenye thamani ya Shilingi bilioni 378.56, ikiwa ni ununuzi wa asilimia 60 ya bajeti ili kazi zianze mapema kabla ya msimu wa mvua kuanza.
Lakini pia, tumeanza utekelezaji wa awamu ya pili ya asilimia 40 iliyobaki katika awamu ya kwanza mikataba 969 imeshasainiwa na kazi zimeshaanza maeneo mbalimbali, Zabuni 1,700 ambazo gharama ya kila zabuni ni chini ya Shilingi bilioni 3 zinatangazwa kwenye ngazi ya TARURA Mikoa na Zabuni 6 ambazo gharama yake ni zaidi ya Shilingi bilioni 3 zinatangazwa katika ngazi ya TARURA Makao Makuu
Kwa upande wake Msemaji mkuu wa serikali na Mkurugenzi mkuu wa idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amesema serikali inaendelea kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha inapeleka fedha za kutosha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya barabara hapa nchini.
Serikali inaendelea kufanya kazi kubwa za kutosha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya barabara nchi nzima ili kuwarahisishia wananchi kutekeleza majukumu yao
Lengo la Mpango Mkakati wa pili wa wakala wa barabara za vijijini na mijini ifikapo 2025/26 asilimia 85 ya mtandao wa barabara za Wilaya chini ya TARURA zitakuwa zinapitika kwa misimu yote na nyakati za mvua hapatakuwa na taharuki itakayojitokeza.
0 Comments