SERIKALI YATENGA BILIONI 22 KWAAJILI YA UNUNUZI WA MITAMBO VIFAA NA UJENZI WA MAABARA YA KISASA

 

📌RHODA SIMBA


KATIKA mwaka huu wa fedha Serikali imetenga sh.bilioni 22 kwa ajili ya ujenzi na ununuzi wa mitambo na
vifaa vya kisasa vya kimaabara.

 Hayo yamesemwa leo  Oktoba  11 jijini Dodoma  na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk.Fidelice Mafumiko wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mamlaka ya   Maabara ya Mkemia  Mkuu  wa Serikali kwa mwaka 2021/22 na vipaumbele vya bajeti ya 2022/23, ambapo amesema  gharama ya kipimo hicho imedumu kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka 10 ni sh.100,000 kutokana na serikali kubeba mzigo wa gharama zingine.

 

Aidha amesema  kwa uhalisia kipimo hicho gharama yake ni sh.700,000 hadi 800,000 kutokana na ughari wa kemikali lakini kwa muda mrefu serikali imebeba gharama hizo ili wananchi wapate huduma 

Zile kemikali zinazosaidia kufanyika kipimo bei zake zipo juu na kuna kemikali moja huwa tunanunua kila baada ya miezi mitatu ni Dola za Marekani 6,000 lakini ikitokea suala la janga huisha kabla ya muda huo.

Amesema kama mtu anataka kupima vinasaba vya baba, mama na mtoto ni Sh.300,000 na wamepeleka mapendekezo serikalini iongezeke kidogo ili kusaidia kuhudumia watu bila kuathiri uendeshaji wa mitambo na gharama za kemikali.

“Sehemu kubwa ya DNA inatumika kwenye masuala ya jinai kama masuala ya ulawiti, ubakaji, au hata wizi, kwa hiyo sio kwamba DNA inatumika kuonesha wazazi halisi lakini inasaidia kwenye masuala hayo ya jinai,”alisema.


 

Kuhusu uchunguzi wa jinsi tata, alisema mamlaka hiyo inapofanya uchunguzi huo huwasilisha matokeo kwa madaktari bigwa walioomba ufanyike.

“Kama inatokea wasiwasi mtu anasema haelewi jinsi yake kama ni ya kike au ya kiume sisi tuna uwezo huo wa kuona hii ni ya kiume au ya kike mara moja, kwa hiyo tunafanya uchunguzi wenye weledi unaotawaliwa na kutunza siri kwa anayefanyiwa uchunguzi na kupeleka majibu kwa aliyeomba kifanyike kipimo,”amesema.

Awali, amesema katika Mwaka wa Fedha 2021/22 vibali vya uingizaji wa kemikali viliongezeka kufikia 63,588 ikilinganishwa na vibali 49,234 vilivyotolewa mwaka wa fedha 2020/21 ikiwa ni ongezeko la vibali 14,354.

“Mbali na utoaji vibali vya kemikali, Mamlaka katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2021/22 imefanikiwa kusajili wadau wanaojihusisha na shughuli za kemikali 1087 ikilinganisha na wadau 1057 waliosajiliwa kwa mwaka fedha 2020/21 ikiwa ni ongezeko la wadau 30,”amesema.


 


Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha huduma na sheria wa mamlaka hiyo, Daniel Ndiyo, amesema mahakama zimekuwa zikitumia ushahidi wa vinasaba na kutoa wito kwa jamii inapotokea mtu amefanyiwa ubakaji au ulawiti asikimbilie kunawa ili kurahisisha upimaji wa kipimo hich

“Huwa zinachukuliwa mbegu za kiume na kuletwa kwa Mkemia ili zipimwe, na kwa wengine ambao huwa wanasababisha ujauzito kwa hiyo mtoto akizaliwa huwa tunaletewa sampuli kwa ajili ya kumpima mama baba na mtoto na kama matokeo hutumika kama ushahidi,”amesema.

Amesema kipimo hicho hutumika kwenye kesi nyingi za mirathi, jinai na ndoa.

 

Post a Comment

0 Comments