FILAMU YA ROYAL TOUR YALETA MATOKEO CHANYA

 


📌RHODA SIMBA

IMEBAINISHWA kuwa juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kuitangaza nchi pamoja na vivutio vilivyomo kupitia filamu maalum ya  Royal Tour matokeo chanya ya filamu hiyo yameanza kushuhudiwa katika mwaka wa fedha wa 2021/22 katika kiwanja Cha Kilimanjaro International Airport (KIA).

Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na ongezeko la abiria kutoka  laki 347,757 mwaka 2020/21 na kufikia abiria  laki 654,159 mwaka 2021/22 ni sawa na ongezeko la asilimia 88.

Hayo yameelezwa  Leo Oktoba 11 jijini Dodoma  na  Mtendaji Mkuu wa  kampuni ya uendelezaji na uendeshaji wa kiwanja Cha ndege Cha Kilimanjaro (KIA)  Christina Mwakatobe wakati akitoa taarifa ya utekelezaji  wa shughuli za KADCO kwa vyombo vya habari.

Amesema kuwa mafanikio mengine ni kupitia shirika jipya la ndege la Eurowings Discover(part of Lufthansa Group)iliyoanza safari zake kutoka Frankfurt,Ujerumani kwenda KIA kuanzia mwezi Juni mwaka huu,shirika hilo linachangia kuongeza idadi ya abiria na mizigo.

Lengo ni kuendelea kuwa na mashirika ya ndege za kukodi(charter flights)ambayo yameendelea kutumia KIA kwa kuleta makundi maalumu ya watalii kutoka sehemu mbalimbili duniani

Kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya Nchi kuwekeza KIA katika maeneo tofauti ikiwemo hotel za kisasa,maeneo ya biashara mchanganyiko(business Complex)na jengo la wageni mashuhuri(CIP lounge facility),"Ameeleza.

Kadhalika amesema kuwa jali ya uendeshaji uliendelea kuimarika hadi mwaka wa fedha 2020/21 ambapo Dunia ilikumbwa na janga la Uviko 19 lililoathiri sekta nyingi za kiuchumi Duniani ikiwa ni pamoja na sekta ya usafiri wa anga.

 


Amesema katika kipindi hicho shughuli za uendeshaji KIA zilishuka kwa kiasi kikubwa kutokana na nchi nyingi kufunga anga ikiwa ni njia moja wapo ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo,hii ilipelekea idadi ya abiria kushuka kwa kiwango kikubwa kutoka laki 794,337 mwaka 2019/20 hadi kufikia abiria laki  347,757 katika kipindi Cha mwaka 2020/21 ikiwa ni punguzo la abiria kwa asilimia 56.

"Kupunguza kwa shughuli za uendeshaji KIA kuliathiri mapato,ikizingatiwa kwa chanzo kikuu Cha mapato ya KADCO ni tozo zinazotokana na abiria wanaopita KIA pamoja na kutua na kuruka kwa ndege kiwanjani,hali hii ilipelekea menejimenti ya KADCO kuchukua hatua ya kubana matumizi na kusimamisha kwa muda baadhi ya shughuli za maendeleo ili iweze kupita Katika kipindi hiki kigumu ikiwa inaendelea kujiendesha,

Hata hivyo nikiri kuwa kipindi hiki tukiendelea kutoa huduma kwa kukidhi viwango vya kitaifa na kimataifa wakati wa janga la Uviko-19 na kutambuliwa kama moja ya viwanja kilichofanya vizuri zaidi katika kipindi hicho kwa kuzingatia maelekezo ya kujikinga yaliyokuwa yanatolewa kupitia Wizara yetu ya Afya,"amefafanua.

Ikumbukwe kuwa Usafiri wa anga ni chachu ya kuwezesha kukua kwa sekta nyingine mtambuka ikiwemo sekta ya Utalii, mifugo,kilimo na biashara ambapo huimarisha shughuli mbalimbali za kiuchumi kupitia mnyororo wa thamani unaotokana na shughuli za uendeshaji wa KIA,mazao mbalimbali ya kilimo na mifugo hupitia KIA kwa ajili ya kwenda kwenye masoko ya nje ya nchi,hii inafaida kubwa katika uchumi wa kanda ya kaskazini na Taifa kwa ujumla.

 

Post a Comment

0 Comments