BODI YA KOROSHO YATOA MIONGOZO YA USIMAMIZI NA UDHIBITI UBORA WA KOROSHO.

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

KAIMU Mkurugenzi wa Bodi ya korosho Tanzania Francis Alfred amesema Bodi ya Korosho imetoa miongozo mingine ambayo ni mwongozo wa usimamizi na udhibiti ubora wa korosho pamoja na Mwongozo wa upatikanaji wa korosho ghafi kwa wabanguaji wa ndani kupitia soko la awali kwa msimu 2022/2023.  

Amesema miongozo yote mitatu tayari imesambazwa kwa Sekretarieti za Mikoa, Vyama vikuu vya Ushirika, Waendesha ghala, wanunuzi na wadau wengine katika mnyororo wa zao la korosho. Aidha miongozo hii inapatikana katika tovuti ya Bodi ya korosho ambayo ni www.cashew.go.tz

Akizungumza leo jijini Dodoma Wakati akitoa taarifa ya utekekezaji wa Shughuli za bodi hiyo kwa mwaka 2021/2022.

Aidha amesema bodi ya Korosho Tanzania ikishirikiana na Bodi ya Usimamizi wa stakabadhi za ghala na Tume ya Maendeleo ya Ushirika zimeandaa na kutoa Mwongozo wa Pamoja wa Usimamizi wa Masoko na Mauzo ya korosho ghafi kwa msimu 2022/2023. 

Amesema bodi tayari imeanza kusajili na kutoa leseni kwa wanunuzi wa korosho ghafi kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi na kubangua nchini ambapo hadi kufikia tarehe 07 Oktoba, 2022, jumla ya kampuni 48 zimejisajili na kati yake, kampuni 18 tayari zimepata leseni na zilizosalia zipo katika hatua mbalimbali za kukamilisha upataji wa leseni," Alisema Mkurugenzi huyo. 

Amebainisha kuwa kwa upande wa minada ya mauzo ya korosho, inatarajia kuanza tarehe 14 Oktoba, 2022 kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani. 

Aidha bodi inatoa rai kwa Vyama Vikuu vya Ushirika kuhakikisha maghala ya vyama vya msingi yanaanza kupokea korosho za wakulima na ghala za minada ambazo tayari zimepata leseni kufungua ghala kwa ajili ya kuhifadhi korosho hizo, tayari kwa mauzo. 

Hata hivyo Bodi ya Korosho Tanzania imekasimiwa jukumu la kusimamia maendeleo ya zao la korosho katika ngazi zote za uzalishaji, ubanguaji/usindikaji, masoko na utafiti ili kuhakikisha kuwa zao la korosho linatoa mchango wake katika kuinua pato la mwananchi na Taifa kwa ujumla.

Amesema bodi itaendelea kushirikiana na wadau wote katika mnyororo wa zao la korosho kuhakikisha mkulima anazalisha na kuuza korosho zake kwa tija kwa maendeleo ya tasnia ya korosho nchini.

 

 

Post a Comment

0 Comments