📌RHODA SIMBA
KAMISAA wa Sensa Tanzania bara Anne Makinda amesema kuwa hadi kufikia septemba 5 2022 kiwango cha kaya zilizohesabiwa nchi nzima na taarifa za kidemographia, kiuchumi na mazingira ni asilimia 99.99 na sensa ya majengo ni asilimia 99.87 ya majengo yote nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tathmini ya zoezi la sensa ya watu na makazi , sensa ya majengo, na sensa ya anwani za makazi ya mwaka 2022 Makinda amesema zoezi la sensa ya watu na makazi limekamiliza rasmi na Rais samia suluhu hassan atatangaza october 2022.
"Kati ya majengo hayo asilimia 100 ya majengo yote yaliyochukuliwa taarifa zake yamehakikiwa anwani za makazi,
Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru wananchi wote kwa ushirikiano wenu wakati wa kutenga maeneo ya kuhesabiwa watu na wakati wa zoezi la kuhesabu watu,nawashukuru viongozi katika ngazi zote kuanzia ngazi ya Taifa hadi mtaa/kitongoji/shehia kwa jitihada zao na ushirikiano wao wakati wote wa kukamilisha awamu hii ya utekelezaji wa sensa,"amesema Makinda.
Aidha amesema kuwa Serikali imehakikisha watumishi wote katika zoezi hilo wamelipwa haki zao zote Kwa mujibu wa mikataba yao ya kazi.
Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali inathamini sana jitihada zao na watabaki kwenye kumbukumbu nzuri ya kuwa miongozi mwa vijana waliochangia maendeleo ya Nchi yetu
Kamisaa Makinda amesema kuwa awamu ya pili imekamilika ya utekelezaji wa sensa na sasa ni awamu ya tatu ambayo ni ya muhimu sana na inajumuisha shughuli zote za baada ya kuhesabu watu.
Kwa upande wake Kamisaa wa Sensa Zanzibar Balozi Mohammed Hamza amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza imefanya sensa 3 kwa wakati mmoja na kwa kutumia TEHAMA ikiwa ni yakihistoria.
Katika historia ya Sensa hii imefanyikia kwa ufanisi na kutumia wataalamu wa ndani hili nijambo la kujivunia kwani ni hatua kubwa kwa maendeleo ya nchi yetu
Balozi Mohammed Hamza
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Albina chuwa alisema kuwa kidunia katika bara la Afrika huwezi kuhesabu kwa asilimia100.
"kisayansi asilima 0.01 ni wale watakaokuja kuhesabiwa sensa ya awamu ijayo na hiyo hainahasara katika kupanga maendeleo ya Nchi,pia katika majengo Haina shida,"amesema Mtakwimu.
Aidha amesema sensa ya majengo ni endelevu Kila baada ya miaka 2,3 na 1 hata zoezi la watu litaendelea kufanyika hata sensa ikikamilika.
Mbali na kumalizika kwa awamu ya pili ya utekelezaji wa sensa Shughuli zinazofata ni pamoja na uchambuzi taarifa za sensa,uzinduzi rasmi wa matokeo ya mwanzo ya sensa na usambazaji wa matokeo ya sensa,taarifa ya mwanzo itahusu idadi ya watu waliohesabiwa Nchi nzima na Kwa jinsia zao katika ngazi zote za utawala na matokeo hayo yatatolewa mwezi oktoba mwaka 2022.
0 Comments