MIGOGORO, wivu wa mapenzi vimetajwa kuwa ni chanzo cha kuwepo kwa ongezeko la Matukio ya mauaji hapa nchini .
Kufuatia hali hiyo Serikali imesema tayari imeunda Tume maalum ya kuchunguza na kuleta majibu kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa leo September 14 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Hamis Hamza wakati akijibu Swali la Mbunge wa Viti Maalum Cecilia Pareso aliyetaka kujua kauli ya Serikali katika kutatua changamoto ya wimbi kubwa la mauaji hapa nchini.
Ameeleza kuwa katika Tume iliyoundwa na Serikali itakaa na kuona kama wataweza kutoa hadharani majibu ya uchunguzi huo.
Wakati huohuo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ameitaka Serikali kuja na majibu sahihi kwa wananchi.
0 Comments