IMEBAINISHWA kuwa watu elfu 33 kwa mwaka wanafariki dunia kutokana na athari za moshi utokanao na kuni pamoja na mkaa wanaopikia ambapo idadi inaonesha ni kubwa kuliko wanaopata ajali na wale wanaofariki kwa ugonjwa wa Ukimwi.
Kadhalika tafiti za kisayansi zinasema kuwa lisaa limoja kwa mtu anayetumia jiko la Moshi kupikia ni sawa na mtu ambae amevuta siagara 300 kwa wakati mmoja.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati January Makamba Jijini Dodoma wakati akizungumza kwa njia ya mtandao katika ufunguzi wa semina ya wabunge wanawake yenye lengo la kuongeza uwezo wa matumizi ya nishati mbadala majumbani.
Makamba amesema kila siku wanawake wengi wanaotumia nishati ya mkaa na kuni kupikia wanameza sumu zinazowaathiri afya zao na kuwaua taratibu.
Mtu wa kijijini leo ukimpima utakuta mapafu yake yapo sawa na anayevuta sigara, kama tupo kijini mtu ameweka mahindi juu ya mafiga ya mbegu ili yasiharibike kwa ule moshi unaoweka weusi ndio huo unaoharibu mapafu ya mpikaji
Makamba
Makamba amesema Nishati ya kuni na mkaa katika matukio mengi ya mimba zinazoharibika sambamba na kuzaliwa kwa watoto njiti yanatonakana na Moshi lakini suala hili limekuwa halizungumzwi katika jamii.
Amesema serikali bado inatafuta jawabu la suala hilo na sera ya Nishati inasema inapaswa kuchukua tahadhali ya haraka kwa wananchi katika kurahisisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa wananchi.
Sisi tumelibeba hili la nishati na kuwapelekea nishati wakina mama vijijini lakini pia na kuweka upatikanaji rahisi wa nishati hizi pamoja na gharama
Makamba
Naye Mkurugenzi kutoka Wakala wa Nishati vijijini REA Hassan Said amesema silimia 90 ya watu wa kijijini wanatumia Nishati ya mkaa na kuni huku changamoto kubwa ikiwa ni upatikanaji wa gesi.
Mama zetu kijijini asilimia kubwa wanatumia mkaa na kuni wengine wana uwezo kabisa wa kupata gesi lakini wanaishi kwa mazoea wengine wanasema wakipikia chakula kwenye mkaa ndio kinakuwa kitamu zaidi kwahiyo semina yetu hii ya wabunge wanawake watatusaidia kupiga kelele ili watu waelewe namna ya kutumia nishati safi ya kupikia,
Amesema lengo la kuanzisha hili ni kuhakikisha wakala wanaosambaza Nishati hizi wanapatikana kirahisi ili wananchi wa vijini watumie lakini kupitia semina hii pia wabunge watatusaidia kupiga kelele
Naye Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu amesema semina hiyo iwaguse wabunge kwenda kupaza sauti kwa jamii ili kuwanusuru wanawake wakatumie Nishati hiyo.
Wanawake wengi ambao wanaathirika na Nishati hiyoo wakiumwa wale wanaosema wanahitaji chakula kitamu cha kwenye mkaa wanawaacha wanaenda kuoa watu wengine naombeni tutoke hapa tukapaze sauti zetu
0 Comments