📌SALMA HAROUN & JOSEPHINE MTWEVE.
Kutokana
na Mchango wa wanawake kuchochea maendeleo na kukuza uchumi nchini Halmashauri
ya jiji la Dodoma inaendesha zoezi la kutoa mafunzo ya kuwakwamua kiuchumi Wanawake
wajasiriamali ili kuleta tija zaidi.
Miongoni
mwa vikwazo vilivyokuwa vinawakumba Wanawake wajasiriamali ni ukosefu wa Elimu
ya matumizi mazuri ya fedha na hivyo kushindwa kufikia malengo.
Afisa
biashara wa jiji hilo, Donatila Donisi, amesema wamekusudia kuelimisha Wanawake
kwa lengo la kurasimisha biashara zao na kuwasaidia kutambulika Serikalini.
Sisi kama Jiji hususani kwenye ofisi ya biashara tumekuja kwaajili ya kuwapa elimu na kuwaambia umuhimu wa ulipaji kodi ili kuwezesha serikali kufanya maendeleo,
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake mkoani hapa, Mary Mbwire
amewashauri wanawake kutumia fursa hiyo kujitokeza kugombea katika nafasi
mbalimbali za uongozi hapa nchini ili kujikwamua kiuchumi na kusaidia wenzao
kujipatia maendeleo.
Tukisikia habari za majukwaa huko mitaani kwetu tusidharau tugombee na kuwasaidia wengine katika nyanja mbalimbali za kimaendeleoMatumaini ya wajasiriamali hao ni kuwa Elimu hiyo itawapatia fursa mbalimbali.
0 Comments