📌 JASMINE SHAMWEPU
ZAIDI ya wagombea
Milioni mbili wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama
Cha Mapinduzi huku Katibu wa Itikadi na Uenzezi akikiri kwamba idadi hiyo ya
wagombea haijawahi kutokea katika chaguzi zote ambazo zimefanyika.
Katibu wa Halmashauri Kuu wa Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi CCM Shaka Hamdu Shaka amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa Habari, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichoketi Jijini hapa chini ya Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan.
Amesema mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi kwa nafasi mbalimbali ndani ya Chama kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Kata na kwa upande wa Zanzibar ngazi ya Jimbo uchaguzi umefanyika vizuri na kwa mafanikio na kwa sasa ni uchaguzi ngazi ya Wilaya.
Pia amesema kutokana na muitikio mkubwa kwa wanachama wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali muda wa kuchukua fomu umeongezwa kwa upande wa nafasi wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Chama cha mapinduzi nafasi 15 Zanzibar na nafasi 15 Tanzania Bara na nafasi za mikoani Tanzania bara na Zanzibar waweze kukamilisha zoezi hilo.
Amesema kila baada ya miaka mitano kwa mujibu ya ibara ya 82 kifungu kidogo cha kwanza Chama kinaekekeza kila baada ya miaka mitano kufanyika uchaguzi wa kuwachagua viongozi ngazi ya Wilaya, wakiwemo wenyeviti wa Wilaya na jumuiya za Chama Cha Mapinduzi
Niseme wazi tangu kuanza kwa mchakato wa uchaguzi ngazi ya shina hadi leo Wilaya zoezi zima limefanyika kwa ufanisi na mafanikio makubwa licha ya changamoto za hapa na pale
Shaka.
Kuanzia tarehe 22 mwezi huu hadi leo September 27 kulikuwa na vikao vya kitaifa kwa maana ya Sekretarieti, Halmashauri ya Taifa, Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa, Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi taifa, Kamati maalumu ya Halmashauri kwa upande wa Zazibar vikao vyote vimefanyika kwa mujibu wa kalenda na vilikuwa vikao maalumu.
Pia amesema Halmashauri Kuu pamoja na mambo mengine imefanya uteuzi wa mwisho kwa nafasi ya wagombea uenyekiti wa ngazi ya Wilaya nchi nzima katika Wilaya 168 kwa Wilaya za kichama.
Amesema wagombea ambao watakwenda kusimama kwenye uchaguzi wa ngazi ya Wilaya kuanzia tarehe 1 hadi 2 Octoba 2022 nchi nzima, hadi sasa maandalizi yameshakamilika.
Hata hivyo amesema Halmashauri Kuu ya Chama cha mapinduzi CCM inatoa rai uchaguzi ufanyike kwa haki na maadili vitendo vya rushwa visitokee na chaguzi hizo zikamilike kwa muda uliopangwa.
0 Comments