MKURUGENZI wa Halmashauri
ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru amesema taasisi mbalimbali kama za kifedha
zina fursa ya kutangaza biashara zao kupitia soko la Machinga Complex linalotarajiwa
kuanza kutumika mwezi wa Septemba mwaka huu.
Mafuru ameyasema hayo
jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya kukamilika kwa mradi wa soko la
wafanyabiashara wadogo maarufu machinga na kufafanua kuwa taasisi hizo zitasaidia
kupata fedha za kutengeneza masoko mengine.
Sambamba na hayo, ametoa
taarifa ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa hoteli ya Dodoma City kwa asilimia
mia moja, na hadi kufikia sasa imeshapata muendeshaji.
Biashara ya hoteli ni ngumu, inahitaji usafi wa kuanzia mashuka, vitanda vya kisasa, vifaa visiharibike. Hivyo inahitaji wataalamu waliobobea wanaoweza kufanya biashara hii kwa weledi. Tulitoa tangazo la kutafuta waendeshaji ambapo kwa sasa tumeshapata
Aidha ametoa wito kwa
watu wenye shughuli mbalimbali mkoani Dodoma kutumia ukumbi wa Jiji uliopo
katika mji wa kiserikali wa Mtumba ambao nao tayari umekamilika na hata baadhi
ya wateja wameanza kuutumia.
Jiji la Dodoma
linaonekana kukua kwa kasi kubwa hasa baada ya serikali kuhamia rasmi, hata
hivyo, licha ya uwekezaji unaofanywa katika ujenzi wa mahoteli na nyumba za
wageni, lakini bado, kunapokuwa na mikutano mikubwa pamoja na vikao vya Bunge, Jiji
hili linaonekana kulemewa kutoka na idadi kubwa ya wageni.
0 Comments