SHERIA YA BIMA KWA WOTE SULUHISHO KUNUSURU NHIF

 


📌RHODA SIMBA


SERIKALI  iimesema ili Mfuko wa  Taifa wa Bima ya Afya usifilisike inakariba kuleta sheria ya Bima ya Afya kwa wote ili wananchi wote waweze kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima hiyo  kutokana na kuwa na idadi kubwa ya Wagonjwa wenye magonjwa yasiyo yakuambukiza.


Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Waziri wa Afya,Ummy  Mwalimu wakati  akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF

Aidha Waziri Ummy amewatoa hofu  wanachana wa Mfuko  huo ,watoa huduma pamoja na watanzania wote kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua stahiki kuhakikisha kuwa Mfuko huo unakuwa imara, endelevu na stahimilivu kwani kwa sasa, ni moja kati ya mfumo unaotumika katika kuhakikisha huduma za afya zinatolewa nchini.

Aidha ameeleza kuwa Mfuko huo pia ndio umekuwa tegemeo la vituo vya kutoa huduma za afya nchini.

"Pamoja na kuwa na wanachama asilimia nane (8) tu ya Watanzania wote, vituo vingi vya kutolea huduma vinategemea mapato kutoka katika Mfuko kwa zaidi ya asilimia 70,

Katika kuhakikisha kuwa maamuzi yote yahusuyo Mfuko huu yanazingatia taratibu na miongozo ya kuendesha chombo hiki, tumefanya tathmini ya uhai na uendelevu wa mfuko kwa mujibu wa sheria na, hivyo tunatambua ni yapi yanapaswa kufanyika ili kuhakikisha mfuko wetu unakuwa endelevu na imara zaidi

Waziri Ummy.  


Kadhalika ameeleza kuwa Matokeo ya awali yanaonesha uendelevu wa Mfuko huo unategemea sana ongezeko la wanachama watakaoandikishwa katika Mfuko huu.

Amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ambayo itaweka mazingira kwa kila mtanzania kuwa na bima ya afya ili kuwezesha dhana ya kuchangiana gharama za matibabu na hivyo kuwaepusha wananchi katika hatari ya janga la umaskini pindi wakiwa wagonjwa au wanapougua. 

"Uzoefu kutoka katika nchi nyingine unaonesha kuwa, kadri idadi ya wanachama inavyokuwa kubwa katika Mifuko hii ya bima za afya za umma kama NHIF, ndipo uwezo wake katika kugharamia matibabu unaongezeka na hivyo kuwa stahimilivu na endelevu kwa muda mrefu,"amesema.

Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na  Samia  Hassan  inaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wananchi wote kuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya karibu na maeneo yao kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa wa ujenzi wa miundombinu ya utoaji wa huduma za afya ikiwemo Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya na Mikoa katika maeneo mbalimbali nchini.

 

 

Post a Comment

0 Comments