📌MWANDISHI WETU
SERIKALI imetangaza msamaha wa kutokushitakiwa kwa mtu yeyote ambaye atasalimisha silaha anayoimiliki isivyohalali katika muda wa miezi miwili uliowekwa.
Akizungumza jijini Dodoma mapema wiki hii jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwezi wa msamaha wa usalimishaji silaha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini alisema kwamba serikali imeweka muda kuanzia 01 Septemba 2022 hadi 31 Oktoba 2022 ili kwa watu kusalimisha silaha hizo.
Naibu Waziri Sagini amebainisha kwamba usalimishaji huo utafanyika katika vituo vya Polisi, ofisi za serikali za mitaa au vijiji. kwamba mtu yeyote atakayepatikana na silaha haramu baada ya muda huo wa msamaha kupita atachukuliwa hatua kama mhalifu mwingine.
Tunafahamu kwamba wapo watu wengine ambao wanamiliki silaha zilizoachwa na ndugu zao ambao wamefariki niwakumbushe kuwa kuendelea kubaki na silaha hizo ni makosa kisheria.Jumanne Sagini.
Sanjari na hilo,Sagini aliwataka pia wale wote waliotajwa kwenye sharia kama makundi maalumu ambao hawaruhusiwi kumiliki silaha pia kusalimisha silaha hizo.
“Kuna wale ambao afya na umri wao hauruhusu kumiliki silaha tunawataka nao wazisalimishe ili zisiangukie katika mikono ya watu isiyo salama na kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.” Alisisitiza naibu Waziri.
Aliongeza kwamba Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wataendesha kampeni maalum ya kitaifa ambayo itashirikisha kamati za usalama za mikoa na wilaya, taasisi za kidini, vyombo vya habari na wadau wengine.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura alisisitiza kwamba hakuna mtu yeyote atakayechukuliwa hatua za kisheria atakaposalimisha silaha kwa hiari.
IGP Wambura alieleza kwamba mtu atakayepatikana na silaha anayoimiliki kwa njia ya haramu baada ya muda huo atachukuliwa hatua za kisheria,hivyo ni vyema kutumia muda uliowekwa kuzisalimisha silaha hizo.
“Serilikali kupitia tangazo lake namba 537 la tarehe 26 June this year,wazisalimishe silaha hizo kwa kuzingatia masharti yaliyopo kwenye tangazo hilo.” Alifafanua IGP Wambura
Pia IGP Wambura amewataka pia wanaomiliki silaha kihalali kuzingatia sheria na kanuni zilizopo ili silaha hizo zisiangukie kwenye mikono ya wahalifu.
IGP Wambura amebainisha kwamba katika kipindi cha miaka mitatu na nusu kuanzia January 2019 hadi June 2022 jumla ya silaha 997 zilikamatwa kutokana na operation mbalimbali za kuzuia na kutanzua ualifu na waalifu.
Katika silaha hizo zipo 52 ziliibiwa kutoka kwa watu wanaomiliki
kihalali,hii inatupa picha kwamba bado kuna silaha zinamilikiwa isvyo kihalali.
IGP Wambura.
Alisema kwamba operation za kuzuia na kutanzua uhalifu ni endelevu hivyo ni muhimu watu wenye silaha wanazomiliki isivyo halali ili kukwepa mkono wa sharia.
0 Comments