📌RHODA SIMBA
SERIKALI kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imebaini watu wanaoendesha vitendo vya kihalifu nchini ni watu waliomaliza vifungo vyao gerezani na kurudi uraiani baada ya misamaha na wengine ni raia wakawaida.
Tamko hilo limetolewa Jijini Dodoma na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni katika Mkutano na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama nchini na hatua zinazochukuliwa.
Amesema kuwa Serikali iko makini katika kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama Nchini na inachukua kwa wahalifu kupitia Jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi na usalama.
Aidha amesisitiza kuwa hatua zinachukuliwa na jeshi la polisi katika kukabiliana na wahalifu hasa vikundi vinavyoua na kupora mali za watu maarufu kama panya road ikiwa ni siku chache kupita kuripotiwa matukio ya uvamizi yanayoendelea nchini kwa baadhi ya maeneo.
"Serikali iko kazini na haitaruhusu kuona wananchi wake wanafanyiwa vitendo vya kihalifu na kufumba macho,muda wote Serikali iko kazini kupitia vyombo vya ulinzi na usalama na mhalifu yeyote atakayebainika atachukuliwa na kupelekwa katika vyombo vya sheria,"amesema Masauni.
Amesema tayari idadi kubwa ya wahalifu wamekamatwa, wazazi wao,wanaoshirikiana nao na wanaonunua vitu vya wizi ili kuisadia polisi ushahidi.
Idadi kubwa ya wahalifu tumewakamata na tunawashikilia pamoja na watu wanaoshirikiana nao katika vitendo vya kihalifu,wananchi mnatakiwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi Ili kukomesha vitendo hiviMasauni.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la polisi Camilius Wambura amesema serikali kupitia Jeshi la Polisi haijawahi kushindwa hivyo wahalifu wakae chonjo na wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo sheria kali zitachukuliwa.
"Serikali kupitia Jeshi la polisi haijawahi kushindwa na jambo lolote hasa matukio ya wahalifu tumekuwa tukipambana nao na tunahakikisha matukio haya yanakoma na watanzania wasiwe na wasiwasi kwani Serikali yao iko macho muda wote,"amesema.
Kuhusu sintofahamu iliyotokea siku za karibuni katika barabara ya mwendo kasi Jijini Dar es salaam IGP Wambura amewaonya madereva wanaovunja sheria nakuagiza sheria kali zichukukiwe.
Amesema kuwa ni lazima sheria ifuate mkondo wake bila kubagua au kumfumbua mtu yeyote macho atakayekiuka masharti na atakaye vunja sheria.
0 Comments