📌RHODA SIMBA
WIZARA ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema kuwa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu jijini Dodoma upo katika hatua ya utekelezaji na tayari Serikali imeshaanza kutenga fedha za ujenzi huo.
Hayo yamesemwa leo September 13 Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Pauline Gekul wakati akijibu Swali la Mbunge wa Morogoro Kusini Innocent Kalogeris
Aidha Kalogeris ameuliza kuwa ni lini ahadi ya ujenzi wa uwanja wa mpira Dodoma iliyotolewa na Mfalme wa Morocco itatekelezwa.
Gekulu amesema Serikali imefuatilia utekelezaji wa ahadi ya ujenzi wa uwanja wa mpira Dodoma iliyotolewa na Mfalme wa Morocco huku akisema mawasiliano kuhusu utekelezaji wa mradi huo baina ya Serikali ya Tanzania na Morocco bado yanaendelea.
Katika kuhakikisha kwamba mradi huu unatekelezwa Serikali imedhamiria kutafuta fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali vikiwemo sekta binafsi na wabia wa maendeleo
Gekul
0 Comments