WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Innocent Bashungwa amesema serikali itahakikisha viongozi wote wanaowahudumia
walimu watasikiliza kero na kutatua changamoto zinazowakabili nchini.
Akiwa
jijini Dodoma, waziri Bashungwa amesema viongozi hao wanatakiwa kuwa karibu,
kuwasimamia, kupokea kero na malalamiko katika maeneo yao ya kazi.
Aidha
amesema serikali itahakikisha wakurugenzi wanawaelimisha walimu kuingia kwenye
mpango wa mafunzo kwenye Halmashauri kwa kuzingatia mwongozo kwa waajiri.
Wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa wahakikishe walimu wanaoingizwa kwenye mpango wa mafunzo na wasikose kuwalipa stahiki zao za mafunzo punde wanapopata udahili
Wakati
huo huo, ameongeza kusema kuwa serikali inaendelea kuboresha vituo vya walimu, ili
kuongeza tija katika ufundishaji na ufunzaji shuleni.
Naelekeza viongozi wa elimu kufuatilia ufundishaji wa walimu darasani na kutatua kero zao katika maeneo yao ya kazi na viongozi waende shuleni kuwahudumia walimu na si kukaa ofisini
Waziri
Bashungwa pia amemwagiza katibu mtendaji wa Tume ya taifa ya walimu kupitia na
kuchambua upandaji wa madaraja kwa kila mwalimu na kubaini stahiki halali ya
daraja na kuwapandisha watakaobainika kucheleweshewa stahiki zao.
Kwa
mujibu wa Waziri Bashungwa amesema kumekua na malalamiko mengi kutoka kwa
walimu kutolipwa stahiki zao za uhamisho, likizo, matibabu na mazishi kwa
sababu zisizoeleweka, kunyimwa vibali vya kwenda masomoni na kutolipiwa gharama
za mafunzo, kutokuwa na mawasiliano mazuri na kutopandishwa vyeo na madaraja
kwa wakati.
0 Comments