SERIKALI imefuta Tozo ya miamala ya kielektroniki ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu na miamala ya simu kwenda benki.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa leo Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu malalamiko ya wananchi kuhusu tozo za miamala ya kielektroniki marekebisho yanayotarajiwa kufanyika ni kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu na simu kwenda benki.
Marekebisho yanayotarajiwa kufanyika ni kama ifuatavyo, kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu na simu kwenda benki
Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja kwenda benki nyingine, kutowahusisha wafanyabiashara wadogowadogo kama ilivyokuwa kwenye kanuni za sasa na kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki
Aidha Dkt. Mwigulu amesema marekebisho hayo yataanza kutumika Oktoba 1 mwaka huu ambapo alisema Rais alisisitiza kupunguzwa zaidi tozo ambapo Wizara ya Fedha ilipunguza tozo zaidi kwa kushusha tena kiwango cha juu kutoka 7,000 hadi 4,000.
Ikumbukwe kuwa tozo hizo ambapo viwango vya tozo vilishushwa kwa asilimia 30 kutoka kiwango cha juu cha shilingi 10,000 hadi kiwango cha juu cha shilingi 7,000, viwango ambavyo vilianza kutumika tarehe 07 Septemba, 2021
Dkt.Mwigulu.
Dkt.Mwigulu amesema sambamba na hatua hiyo, Serikali inafuta utaratibu wa kodi ya zuio inayotokana na pango kukusanywa na mpangaji na badala yake jukumu hilo linarejeshwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa utaratibu utakao bainishwa kwenye kanuni.
Napenda kusisitiza kuwa kodi ya zuio ya pango siyo ya mpangaji bali inapaswa kulipwa na mpangishaji ambaye ndiye anapokea mapato kutokana na uwekezaji au biashara ya kupangisha
Utaratibu huo umekuwa ukitumika kwa muda mrefu kwenye nyumba za biashara na nyumba zinazopangishwa kwenye makampuni au mashirika yanayofunga ritani za kodi,"amefafanua Waziri wa Fedha.
Amesema itakumbukwa kuwa, katika mwaka wa fedha 2021/22, Sheria ya Malipo ya Taifa, Sura na. 437 (National Payment System Act, Cap. 437) ilifanyiwa marekebisho kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2021 na kuanzisha tozo ya miamala ya kutuma na kutoa fedha kwa njia ya simu za mikononi yaani, Mobile Money Transaction Levy.
Sambamba na tozo hii, tulipandisha tozo kwenye mafuta kwa ajili ya kutunisha mfuko wa TARURA na Mfuko wa Elimu ya juu, Lengo la kuanzisha tozo hizi ni kuunganisha nguvu na umoja wa Watanzania wote katika kuiwezesha Serikali kuongeza kasi ya kutekeleza miradi hasa ile iliyokosa fedha kutokana na ufinyu wa bajeti ili kuwakwamua wananchi dhidi ya ukosefu wa huduma za jamii-msingi kwa kuzingatia kuwa sura ya bejeti yetu karibu kila mahitaji ni mahitaji ya lazima
Mahitaji ya lazima yanayolindwa kwa mfano SGR, TANROADS, Bwawa la Umeme, REA, TARURA, Maji, Elimu, Mikopo ya Elimu ya Juu, Elimu bila Ada, Mishahara, Deni la Taifa, Afya ni takribani 27.9 trilion na makusanyo ya ndani ni takribani 28.01trilioni,"amesema.
Serikali haina malengo ya kutoza wananchi wake kodi/tozo kwa ajili ya kuwapa mzigo tu, bali inalenga kuwahusisha Watanzania wote kwa umoja wetu katika juhudi za kujikwamua kimaendeleo.
0 Comments