SACP MUTAFUNGWA:MADEREVA WA SERIKALI HAWAPO JUU YA SHERIA,AWATAKA KUJITAMBUA

 


📌RHODA SIMBA

IMEELEZWA kuwa ili kudhibiti ajali elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa Serikali iendelee kutolewa kwa kuwajengea uwezo wa kujitambua kama watumishi wa umma wanaopaswa kulinda uhai wao na wateja wao kwa kuheshimu na kutii sheria.

Akizungumza katika mafunzo maalumu ya elimu ya Usalama barabarani kwa madereva wa magari ya viongozi wa Serikali na waheshimiwa wabunge leo jijini Dodoma,Kamanda wa Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani SACP Wilbroad Mutafungwa alisema madereva hao wanapaswa kujitambua kuwa hawapo juu ya sheria na wanapaswa kutii sheria kama madereva wengine.

"Wajue wanadhamana ya maisha ya viongozi wao na Mali za umma wanatakiwa kutambua udereva ni taaluma na ndio sababu wakapata Ajira katika kada hiyo

Waache kutumia vyeo na ukuu wa viongozi wao ambao sio madereva wa magari ya serikali kwani wameajiliwa kwa majukumu mengine na sio udereva tu

Kamanda Mutafungwa.


Aidha amewataka kutumia mbinu mbalimbali za udereva wa kujihami kwa kutambua nafasi zao lakini kujitambua kiafya,kisaikolojia na nafasi zao katika jamii na utumishi wa umma.

"Dereva wa gari la Serikali anapaswa kuwa mtulivu na mwenye kujitambua kwani taaluma ya udereva inahitaji utulivu kwakuwa inabeba dhamana ya maisha ya watu,

Derava hapaswi kuwa anamihemko na anatakiwa kujiepusha na makando kando yanayoweza kupelekea apoteze weledi katika kazi zake,mfano:kuacha ulevi na matumizi ya kilevi Cha aina yoyote Ile na kuheshimu sheria ya mwendokasi,"alisema.

Katika hatua nyingine kamanda Mutafungwa amesema wataendelea kusimamia sheria bila kumuonea Dereva yeyote.

"Atakaye patikana kutoheshimu sheria hatua za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kama sheria zinavoelekeza,tutawafungia au kuwafutia leseni za udereva madereva sugu wasiofundishika,"alisema.


 

Kwa upande wake Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Jumanne Sagini amesema mafunzo hayo yawe endelevu kutokana na umuhimu wake huku akishauri waratibu wa mafunzo hayo wazingatie ratiba za madereva kutokana na ratiba za majukumu yao.

“Ikiwezekana mafunzo hayo yafanyike siku za mwishoni mwa juma ili madereva wengi waweze kuhudhuria na kupata mafunzo hayo yatakayowasaidia katika kutekeleza majukumu yao" alieleza.

 

Post a Comment

0 Comments