HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa NEC imewateua wagombea mbalimbali wa nafasi ngazi ya Wilaya Nchini huku ikiongeza muda wa kuchukua fomu na kurejesha kwa nafasi ya UNEC wa Chama hicho.
Pia Chama Cha Mapinduzi CCM kimetoa wito kwa wagombea kuhakikisha wanafuata maadili kwa kujiepusha na rushwa ili Haki iweze kutendeka.
Hayo yameelezwa hii Leo na Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM,Taifa Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na uteuzi wa Wagombea hao ngazi ya Wilaya ambapo amesema kuwa Chama kitahakikisha kinafuatialia kwa karibu chaguzi zote ili kuhakikisha Haki inatendeka.
Shaka amesema kuwa Halmashauri Kuu katika kikao chake kilichoketi Leo chini ya Mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mambo mengine wameongeza muda wa kugombea nafasi hizo kutokana na wanachama kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania nafasi za uongozi.
Amesema kuwa muda wa uchukuaji fomu na urejeshaji wa fomu kwa wanachama wa CCM nchini itatolewa kuanzia Otoba Mosi hadi tano mwaka huu.
Katika hatua nyingine Katibu mwenezi huyo ameeleza kuwa mwitikio wa wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama hicho ni mkubwa kuliko miaka yote kwani mwaka huu idadi ya wagombea imefikia takribani milioni mbili nchini kote.
0 Comments