MKURUGENZI JIJI DODOMA: WAMACHINGA WOTE WAHAMIE MACHINGA COMPLEX IFIKAPO SEPTEMBER 23

 


📌RHODA SIMBA

UONGOZI wa Jiji la Dodoma umewataka Wamachinga wote waliopo katika Jiji hilo kuhakikisha wanahamia kwenye Soko jipya la Kisasa la Machinga Open Market lililopo eneo la Bahi Road ifikapo Septemba 23 Mwaka huu huku ukisema uhakiki wa machinga hao unaendelea kufanyika.

Aidha Mkurugenzi  wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru amesema,kutokana na wamachinga kuendelea kujitokeza kila siku,Jiji la Dodoma limepanga kuendelea kujenga masoko kama hayo katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini humo,Mafuru alisema shughuli ya kuwahamisha wamachinga tayari imeshaanza huku septemba 23 mwaka huu ndio itakuwa mwisho wa wamachinga kuonekana wakifanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi.

"Kuanzia Leo Watu wanaanza kuingia kwenye soko la wamachinga,kwa hiyo kuanzia Septemba 24 mwaka huu hatutamwona Machinga yeyote nje ya soko lile. “alisema MafuruDodoma manunuzi yote Watu wajue yatafanyika kwenye soko la wamachinga " amesema Mafuru

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo,uwezo wa soko hilo ni kuchukua wamachinga 5000,lakini mpaka sasa uhakiki unaonyesha wapo wamachinga 3000,maana yake waliopo mtaani wanaondoka wote hakuna atakayebaki nawatakapokuja wapya tutawajazia pale kwa kuzingatia wale tu wenye sifa za kuingia pale.”amesisitizana kuongeza kuwa

Kwa hiyo yeyote hata kama ndio unaanza leo utaingia kwenye soko na hata kama utakosa pale utaingia kwenye masoko tuliyoyaandaa ila utaratibu ni kwamba kwa wale tuliowasajili mwanzo watatangulia ,na wale wanaoongezeka tutaendelea kuwapokea.

Hata hivyo alisema mpaka sasa hatujapata malalamiko ya watu ambao hawajahakikiwa na zoezi la uhakiki halijawahi kufungwa huku akisema,hata sasa bado wanaendelea kuwapokea na kuwahakiki kwa lengo la kupata nafasi.


 

“Lakini tunajua hii ni ajira ,sasa kwa wale watakaoongezeka  watenda kwenye ‘D  centers’  zetu,wengine wanaoendelea kuongezeka jiji litajenga masoko mengine ya wamachinga eneo la Nzuguni pamoja Mnadani.

Amesema,makusanyo yatakayotokana na soko hilo yatatumika kujenga masoko mengine yenye mfano wa soko hilo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma ambayo wamachinga wataendelea kuwekwa na kufanya biashara kwenye masoko hayo.

Kufuatia kukamilika kwa soko hilo amesema,hatarajii kuona mfanyabiashara anafanya shughu

li zake katika maeneo yasiyo rasmi na kwamba wafanyabiashara wote wanapaswa kwenda kufanya biahsra katika soko hilo ambalo limejengwa kwa ajili yao.

Mafuru alisema,kuanzia tarehe hiyo,manunuzi yote yatakuwa yanafanyika katika soko la Wamachinga na siyo kwenye mitaa kama ilivyozoeleka .

“Ujenzi wa Soko  umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 9.53 mpaka kukamilika kwake ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alitoa shilingi bilioni 3 na sisi kama Jiji tulitoa kiasi cha shilingi bilioni 6.5 Kwa kutumia mapato ya ndani kuongeza na kufikia kiasi hicho kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa soko hilo.”amesema Mafuru

Amesema , katika soko hilo kumewekwa  mfumo wa kisasa kwa ajili ya Wafanyabiashara hao wadogo wadogo ambapo kwa sasa wameanza kufanya uhakiki ili kupata watu waliolengwa kufanya biashara katika soko hilo.


 

Vile vile alisema,zimefungwa kamera za kisasa za kudhibiti wizi huku akisema katika soko hilo hakutakuwa na wizi kwani kila atakayefanya uhalifu wowote atabainika mara moja.

Mkurugenzi huyo amesema,kukamilika kwa soko hilo kunakwenda kulifanya jiji la Dodoma kuwa safi.

" Tuligundua hata viongozi wa juu Wafanyabiashara ndogo ndogo Kwa namna Moja ama nyingine walifanya mji uonekane haupendezi . "

 

Post a Comment

0 Comments