📌RHODA SIMBA
WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamadi Masauni amesema Serikali inaendelea kutoa haki mbalimbali za msingi kwa wafungwa walioko magerezani kwa mujibu wa sheria.
Masauni ameyasema hayo Leo jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Bahati Ndingo aliyehoji ni lini Serikali itaweka mfumo utakaoruhusu wafungwa kupata haki ya faragha.
Akijibu swali hilo Mhandisi Masauni amesema Tendo la ndoa ni haki lakini sio haki ya msingi.
Haki ya msingi tunayotoa kwa wafungwa ni chakula, mavazi, malazi, Kuna mambo mengi ambayo yanapaswa kufanyika kwanza kabla ya kuruhusu haki hiyo gerezani
Haki hiyo itaanza kutolewa pale ambapo mifumo ya kisheria, na miundo mbinu ya magereza itakapokidhi kutolewa kwa haki hiyo lakini pia na masuala mengine yatakayozingatiwa ni usalama,mila na desturi za watanzania, kwani haki hiyo inatakiwa kutekelezwa kwa faragha
Mhandisi Masauni
0 Comments