WAFANYABIASHARA
wadogowadogo maarufu kama machinga wa Jiji la Dodoma wametakiwa kuhamia katika
soko la machinga complex liliopo Bahi road kuanzia sasa hadi tarehe 23 Septemba
mwaka huu ambapo ujenzi huo umefikia asilimia 100 utakaoweza kuwasaidia wamachinga kufaidika kupitia mradi huo.
Mradi
huo umegarimu takribani bilioni 9.53 ambapo wamachinga 3000 wanatarajiwa
kuingia katika soko hilo ifikapo tarehe hiyo iliyopangwa kwa lengo la kuwafanya
wafanyabiashara wakopesheke.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru amesema wamachinga
wataweza kufaidika kutokana na faida zitakazopatikana katika soko hilo.
Amesema
wamachinga watakua katika mpangilio maalumu uliopangwa utakaoweza kusaidia
kufikiwa kwa urahisi katika kupata mikopo itakayo wasaidia katika biashara zao
Mradi huu utasaidia kujulikana eneo lako ni lipi n akutambulika kuwepo katika mifumo ya benki itaweza kuwasaidia wamachinga katika kupata mikopo,
Aidha
ameongeza kwa kusema kuwa soko hilo lina uwezo wa kubeba wamachinga 5000 kwa
kusudi la kufanya manunuzi yote kufanyika katika soko la Machinga Complex ikiwa
kama agizo la Mh Rais alivyoweza kuagiza Jiji la Dodoma kuwa safi.
0 Comments