LST YAWATAKA WAHITIMU WA SHERIA KUFANYA MAFUNZO YA UANASHERIA KWA VITENDO.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MKUU wa kitengo cha sheria katika Taasisi ya Mafunzo ya uanasheria kwa Vitendo (LST) Berinda Mollel amewataka wahitimu wote wa shahada ya sheria kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali wanaotarajia kufanya kazi kama mawakili binafsi nchini au katika utumishi wa umma kufanya mafunzo ya mwaka mmoja katika taasisi hiyo huku akiainisha kuwa wahitimu hao ni wale waliomaliza shahada zao baada ya sheria kuanza kufanya kazi mwezi Mei 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma katika mkutano mkuu wa mawakili  ulioenda sambamba na uzinduziwa Chama Cha Mawakili   nchini amesema lengo la taasisi hiyo ni kutoa mafunzo bora na stahili ya uanasheria kwa vitendo, utafiti na ushauri elekezi katika masuala ya sheria kwa watu stahiki.

Dhamira kuu ya taasisi hii ni kutoa ushauri wa kisheria kwa watoto, kutoa ushauri wa kisheria kwa wanawake, kuandaa nyaraka za mahakamani, kufuatilia mwenendo wa kesi mahakamani,
 kutoa mwongozo wa taratibu za kufuatilia kesi, kutoa msaada wa kisheria katika makundi mengine sambamba na usuluhishi wa migogoro

 Mollel

Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo imeweza kupata mafanikio kama wahitimu wa taasisi wamekuwa wakiorodheshwa/kusajiliwa kama mawakili wa kujitegemea na wengine wakiajiriwa katika utumishi wa umma kama mawakili wa Serikali au Mahakimu wakazi.

Aidha wahitimu wengine wanaendelea kukamilisha taratibu za kuwa mawakili wa kujitegemea ili waanze kufanya kazi kwa weledi.

Kuna watu wanatoka vyuoni moja kwa moja wanakuwa hawafahamu namna ya kufanya kazi hizi kwahiyo Taaisi yetu sisi inawapa mafunzo lengo ni kuwajengea uwezo mawakili hawa ili waliendelee kutekeleza majukumu yao.

Mollel.

 

 

Post a Comment

0 Comments