KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA UJENZI WA MAABARA YA TAIFA YA ATOMI MAKAO MAKUU DODOMA



📌RHODA SIMBA

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii,imeridhishwa na ujenzi wa maabara ya Taifa ya Atomi huku ikiiagiza Tume ya nguvu za Atomi kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ifikapo Septemba 30 mwaka huu ili ianze kutumika kwa manufaa ya Umma na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua maabara na Ofisi za Tume hiyo,Mwenyekiti wa kamati hiyo Stanslaus Nyongo amesema kuwa uwepo wa maabara hiyo itarahisisha upimaji wa baadhi ya bidhaa  ambazo  zinatumia  mionzi ikiwemo na suala la usalama wa nguvu za Atomiki kwa ujumla.

“Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ambao ndio wasimamizi wa jengo hili ndio tumekuja kuliona na sisi  leo hii kamati ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya jamii tumekukagua  jengo hili limefikia asilimia 85 ya ujenzi  tumeridhika na ujenzi wa jengo   tunaipongeza Wizara ya Elimu na Rais wetu pia ambae ametoa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 3.8 kwaajili ya jengo  hili,

Na kama ilivyo kawaida ya maazimio ya Serikali kuwa Taasisi zote zihamie jijini Dodoma  mpaka mwezi wa 11 mwaka huu 2022  linaenda kukamilika na watahamia hapa  na wale wote ambao watataka kupimiwa mionzi kwenye bidhaa zao  muda si mrefu huduma hii itaanza kutolewa
Stanslaus Nyongo



Nyongo ambaye pia ni Mbunge wa Maswa Mashariki ameitaka Tume hiyo ya nguvu za Atomiki kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia   iwaambie watanzania kwa kutoa Elimu kuhusu  huduma wanazotoa kwa lengo la kufahamu na kuitumia maabara hiyo.

Naye Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa  Adolf Mkenda amesema amepokea maelekezo yaliyotolewa na kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma Za maendeleo ya Jamii na kuahidi kuyatekeleza kwa wakati na kwamba Tume ya nguvu za Atomiki ni muhimu hasa katika suala la usalama wa nchi na kuahidi kuendelea  kuwekeza katika Ofisi zote za Kanda za Tume hiyo..

“Nguvu za Atomiki ni muhimu sana  ukiacha maendeeo ya kisayansi katika masuala ya nyuklia lakini wanatusaidia katika kuhakikisha kuwa panakuwa na usalama katika vifaa vya hosptali lakini katika bidhaa ya vyakula pia ambavyo vinaweza vikawa vimekutana na mionzi hatari nguvu hii itawezeshwa kwa kuhakikisha ofisi ya  kanda zote maabara ifanye vizuri pia kuwaendeleza wana sayansi wetu katika masuala ya nyuklia” amesema Profesa Mkenda.

Awali Mkurugenzi Mkuu  wa Tume ya Atomi Profesa  Lazaro  Busagala ameeleza faida ya maabara hiyo pindi itakapokamilika ni pamoja na kuendeleza uzalishaji wa sekta ya nyuklia nchini.

“Tunapata faraja kuona kamati ya bunge inafurahia kuona  ujenzi wa jingo hili unaenda kukamilika,  imefurahishwa kuona kazi inajengwa kwa kiwango kikubwa,  tunaenda kuweka salama maisha ya wananchi lakini pia kuendeleza sayansi ya nyuklia  ambayo inafaida kubwa sana hapa nchini katika sekta ya kilimo, afya, maji pamoja na mifugo”amesema  Busagala

Hata hivyo ikumbukwe kuwa Tume ya nguvu ya Atomi  kwa Sasa Makao Makuu yake yapo Mkoani Arusha ambapo kazi yake kubwa ni kudhibiti matumizi mabaya ya mionzi.

 

Post a Comment

0 Comments