JUMLA YA SH BILIONI 998 KWA AJILI YA VIJANA KUKOPESHWA NA KUJIKWAMUA KIUCHUMI

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

NAIBU Waziri kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, kazi ajira na watu wenye ulemavu Patrobas Katambi amesema kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 998.1 kwenda sehemu mbalimbali ili vijana waweze kukopeshwa na kujikwamua kiuchumi.

Pia amesema Serikali imeendelea kuboresha maeneo ya biashara ili vijana kuweza kuingia katika shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa mikopo.

Ameyasema hayo leo September 15 2022 wakati akifungua Mdahalo kuhusu upatikanaji wa mitaji ya kukuza shughuli za kilimo biashara kwa vijana mdahao ulioandaliwa na Taasisi ya Uendelezaji wa Mifuko ya Masoko ya Kilimo Tanzania (AMDT).

Katambi amewataka vijana kuwekeza kwenye kilimo kwani Kilimo ndio uti wa mgongo.

Amesema vijana wengi wamekuwa wakijikita katika shughuli zisizokuwa na tija na kusahau kuwa shughuli ya msingi kwa vijana kwa sasa ni kwenye kujikita katika nyanja za kilimo Bora na chenye tija.

Tumegundua   kuna haja ya Mtaala wetu wa elimu kubadilika ili uendane na sisi au hawa vijana wetu ili tuwasaidie ninyi wadau AMDT kutumia nguvu kubwa kuwafundisha vijana namna ya kupata mitaji ya kukuza shughuli za kilimo.

Katambi ameongeza kuwa Mtaala wa elimu ubadilike na kumfanya kijana kuweza kujiajiri na sio kusubiri kuajiriwa na badala yake tunataka njia ya aliyemaliza chuo awe na ujuzi na maarifa ya kujitengenezea uchumi wake na Taifa kwa ujumla.

Niwapeni siri ili ufanikiwe katika maisha unatatakiwa uwe na Maarifa ya kutosha, ujuzi wa kutosha pamoja na kipaji

Katambi.

Amesema hata Rais Samia Suluhu Hassan anatambua umuhimu wa vijana na ndio maana anawapa nafasi vijana katika nyanja mbalimbali za uongozi.

Kwa Upande wake mshiriki Theresia Deoscory kutoka Mkoa wa Rukwa amesema katika  Mdahalo huo ulioandaliwa na AMDT ameweza kutambua kuwa fursa nyingi zinazotolewa na Serikali kwaajili ya vijana, hivyo ni wakati sasa wa vijana kuchangamkia fursa na kuacha kuzubaa kwa kujiunga na vikundi katika Kata na Mitaa yao ili waweze kupata fursa hizo za mikopo.

Naye Romanus Mwakimata Mkurugenzi Mtendaji wa LIMA AFRICA COMPANY LIMITED Tabora amesema anajivunia kuwa katika sekta ya kilimo kama kijana na kupitia mdahao huo amejifunza mengi juu ya upatikanaji wa mitaji ya kukuza shughuli za kilimo.

Mwakimata amesema fursa kubwa katika kuinua uchumi wetu sisi kama vijana na Taifa kwa ujumla ni baada ya serikali kushusha Pembejeo za kilimo hivyo basi vijana wasisite kujikita katika shughuli za kilimo Pembejeo zitapatikana kwa bei nafuu.

 

Post a Comment

0 Comments