FAMILI YASUSA KUCHUKUA MWILI HOSPITALI, MAGEREZA YATUHUMIWA KWA KIFO HICHO

📌SAIDA ISSA 

KATIKA hali isiyo ya kawaida familia ya Richard Bukombe iliyopo Miyuji Jijini Dodoma imesusia kuchukua mwili wa ndugu yao katika chumba cha kuhifadhia maiti huku wakilituhumu Jeshi la Magereza kuhusika na kicho hicho.

Aidha Richard Bukombe aliyefahamika kwa jina  maarufu la Baba Paroko aliuawa September  13 na mwili wake  kutelekezwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya familia  Mdogo wa marehemu Bulole Bukombe Jijini hapa amesema kwa mujibu wa mashahidi wa tukio hilo walisema gari la magereza linahusika na chanzo cha ajali hiyo huku wakiiomba Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kulifuatilia suala hilo na kuwapatia majibu ili waweze kuzika mwili wa ndugu yao.

Akizungumzia tukio hilo amesema kuwa marehemu Richard Bukombe, aligongwa na gari mali ya Jeshi la Magereza (Rand cruzer pick up) Septemba 13, mwaka huu jirani na eneo la Twiga hotel Msalato Jijini hapa.

Amesema, marehemu aligongwa na gari hilo mali ya Magereza majira ya saa 12:30 ambapo baadhi ya askari wa jeshi hilo walimchukua na kuondoka naye.

Baada ya kugongwa na kuchukuliwa na watu wa magereza ikabidi mtoto wa marehemu usiku wa Septemba 13, alienda kufuatilia katika maeneo mbalimbali na alipofika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ameuliza mapokezi hakupata taarifa zake lakini alipokwenda katika chumba cha kuhifadhia maiti aliukuta mwili wa baba yake ukiwa umeandikwa  ‘un known’ (mtu asiyefahamika) ndipo akamweleza muhudumu kuwa yule ni baba yake ndipo mwili ukaandikwa jina lake

Kadhalika amesema baada ya tukio hilo kutokea yeye pamoja na  wenzake walipatiwa taarifa na mtoto wa marehemu kuwa kaka yao amegongwa na gari na amekutwa chumba cha kuhifadhia maiti akiwa ametelekezwa.

Mimi nilikuwa Kaliuwa na mwenzangu alikuwa Kibaha ilitubidi kuja kufuatilia tukaanzia Polisi hatukuta taarifa yoyote kuhusu marehemu lakini pia katika hospitali kitabu cha mapokezi tuliangalia taarifa za Sepetemba 13 hadi 15 hatukuzipata taarifa za kupokelewa kwa ndugu yetu tulivyo uliza kwa muhudumu wa chumba cha maiti akasema kuwa ndugu yetu aliletwa na watu jeshi la Magereza

Kutokana na hali hiyo amesema familia inachokitaka kwa hivi sasa ni Wizara ya Mambo ya Ndani kuwapatia majibu ili kuindolea familia sintofahamu iliyopo hivi sasa.

Kama Magereza walimpeleka ndugu yetu katika hospitali hii kwanini wanaficha utambulisho wao na hali hii inatufanya sisi familia kuamini kuwa ndugu yetu kifo chake wao wanahusika nacho inawezekana hata alipogongwa hakufa lakini wao walimmalizia ili kupoteza ushahidi.
Lakini hakuna ripoti yoyote iliyotolewa na daktari ya kifo cha ndugu yetu wala cheti cha udhithibitisho wa kifo cha ndugu yetu hivyo tunaomba majibu ya maswali yetu ili tuweze kuuchukua mwili wa ndugu yetu kwa ya maziko

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma Dk. Nassoro Ibenzi amekiri kuwepo kwa mwili huo katika chumba cha kuhifadhia maiti lakini hakuna taarifa zozote zinazo onesha kupokelewa kwake.

Kweli mwili huu upo hapa lakini hakuna taarifa zozote ambazo zinaonesha kuwa ulipokelewa hapa huu ni uzembe wa watu waliokuwepo wakati marehemu akiletwa hapa

Mkuu wa Gereza la Msalato jijini hapa, alipoulizwa kuhusu tukio hilo amesema kuwa analifahamu kama ambavyo watu wengine wanalifahamu ila watu wa kulitolea ufafanuzi ni Magereza makao makuu.

Watu ambao wanaweza kulielezea sula hili vizuri ni watu wa makao makuu mimi nalifahamu kama ambavyo wewe unalifahamu hivyo makao makuu ndiyo wanaweza kukupa hadithi yote ya suala hilo

Mwambije

 

Post a Comment

0 Comments