📌JOSEPHINE MTWEVE
SPIKA wa Bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amewaomba wadau wa watetezi wa watu wenye ulemavu kuishauri serikali kurekebisha mitaala mbalimbali ya elimu iendane na mazingira ya kundi la walemavu.
Dkt.Tulia ameyasema hayo Jijini Dodoma katika Mkutano wa Shirika lisilo la Serikali la Child Support Tanzania lilipokutana na wadau wa Elimu jumuishi kujadili vikwazo vinavyoikabili kundi la watu wenye ulemavu kwenye sekta ya elimu.
Ameorodhesha changamoto zinazokabili kundi hilo kuwa, ni pamoja na uhaba wa miundombinu rafiki mashuleni ,vifaa visaidizi vya kufundishia , pamoja na uratibu endelevu wa kugharamia elimu jumuishi.
Watoto walemavu mahitaji yao ni zaidi ya wale wakawaida kwahiyo lazima shule ambazo wapo zitazamwe kitofauti kidogo kwasababu changamoto hizi zisipofanyiwa kazi lengo la watoto wote wako sawa hatutalifikia.
Dkt.Tulia
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Noelah Msuya amefafanua kuwa licha ya serikali kutoa vifaa visaidizi,bado havikidhi mahitaji ya watoto wenye mahitaji Maalum.
Mkutano huo ulioratibiwa na Shirika lisilo la Serikali linalotetea watoto wenye ulemavu la Child support Tanzania, ni sehemu ya ukusanyaji wa maoni ili kuboresha Sera ya elimu nchini.
0 Comments